| Tazama watoto hawa wakiwa na mwl wao |
Baadhi ya mikoa Tanzania haina walimu wa kutosha
Shirika lisilo la kiserikali la haki elimu limesema utafiti wake umebaini kuwa mikoa ya kanda ya magharibi nchini humo na ile iliyopo ziwa Victoria haijafikia malengo ya kitaifa ya idadi ya walimu katika kila shule
Katika ripoti hiyo ya utafiti wa shirika la Hakielimu, imeeleza kwamba mgawanyo wa walimu wapya haujalenga uhaba wa walimu uliopo.
Shirika hilo linasema kuwa baadhi ya mikoa iliyopokea mwalimu mmoja kwa kila wanafunzi 37, imeongezwa walimu jambo ambalo sio sawa kwa sababu baadhi ya mikoa haina walimu wa kutosha na hilo linapaswa kuzingatiwa.
Haki elimu wanasema sababu hizo ni baadhi ya mambo yanayochangia ufaulu duni , ambapo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ufaulu kwa shule za msingi umekuwa ni wastan wa asilimia 60 hadi 40 tu.
Limeongeza kwamba walimu wanataka kuishi katika mikoa ya karibu na hivyo kufanya kila wawezali kuwashawshi wadau kutowapeleka mikoa ya mbali.
Hata hivyo ripoti hiyo imetofautisha walimu wa sasa na wale wa miaka iliyopita. Linasema kuwa walimu wa zamani walikuwa na haiba, uzalendo na kujitolea kufanya kazi na pia walithaminiwa sana na jamii lakini leo kazi ya ualimu imekuwa kazi ya ilimradi
Baadhi ya mikoa nchini Tanzania imebuni mbinu zinazoweza kuwavutia walimu ili wafanye kazi katika maeneo yao kutokana na maeneo hayo kuko
0 comments:
Chapisha Maoni