eliaonesmo@gmail.com
Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
IMEELEZWA KUWA MOJA YA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA FILAMU YA ROYAL TOUR NI KUONGEZEKA KWA WATALII KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIA.
HAYO YAMEBAINISHWA LEO JIJINI DODOMA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA UENDELEZAJI NA UENDESHAJI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA KILIMANJARO(KADCO) BI CHRISTINE MWAKATOBE WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI IKIWA NI MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA TAASISI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA CHA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.
AIDHA BI CHRISTINE AMESEMA PAMOJA NA KUONGEZEKA KWA ABIRIA PIA FILAMU HIYO IMESAIDIA KUONGEZEKA KWA MIRUKO YA MASHIRIKA YA NDEGE YA KIMATAIFA.
"KWA MFANO KLM ILIKUWA INAKUJA KILIMANJARO MARA TANO KWA WIKI,MWEZI ULIOPITA SEPTEMBER,SASA INAKUJA MARA SITA KWA WIKI,LAKINI NISEME TU SHIRIKA LA NDEGE KATAR AIRWAYS AMBALO LINAKUJA KILIMANJARO MARA 12 KWA WIKI,KUNA SIKU LINAKUJA ASUBUHI NA JIONI KUNA SIKU LINAKUJA MARA 1 KWA SIKU,LAKINI KUANZIA TAREHE 17 MWEZI HUU KATAR AIRWAYS ITAKUWA INAKUJA MARA 3 KWA WIKI KILIMANJARO,SAMBAMBA NA HILO NI KUENDELEA KUWA NA MASHIRKA MBALIMBALI YA NDEGE ZA KUKODI AMBAYO YAMEENDELEA KUTUMIA KIA KWA KULETA MAKUNDI MAALUM YA WATALII KUTOKA MAENEO MBALIMBALI KAMA NDUGU ZETU WA ISRAEL NA UARABU".
AKIZUNGUMZIA MIPANGO WALIYOJIWEKEA KATIKA MWAKA HUU WA FEDHA WA 2022/2023 NI PAMOJA NA KUONGEZA IDADI YA ABIRIA KWA ASILIMIA 18,KUONGEZA KIWANGO CHA MIZIGO KWA ASILIMIA 16 ,PAMOJA NA KUNUNUA MITAMBO YA KISASA ILI KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA NDANI YA KIWANJA HICHO.
"KUONGEZA MASHIRIKA MAWILI MAPYA YA NDEGE YA KIMATAIFA YATAKAYOTUMIA KIWANJA CHA KIA,HII NI MIKAKATI YA KILA SIKU KUHAKIKISHA TUNAYAVUTIA MASHIRIKA YA NDEGE YAWEZE KUTUA MOJA KWA MOJA KWENYE KIWANJA CHETU CHA KIA,VILEVILE TUNA MALENGO YA KUKAMILISHA MIRADI YA UKARABATI NA UPANUZI WA ENEO LA MAEGESHO YA MAGARI KUTOKA UWEZO KUHUDUMIA MAGARI 83 MPAKA 200,KUNUNUA MAWILI YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 3.6 ILI KUBORESHA HUDUMA KIWANJANI HAPO".
KATIKA HATUA NYINGINE AMETAJA MAFANIKIO AMBAYO YATAPATIKANA KWA TAIFA KUTOKANA NA UENDESHAJI WA KIA KUWA NI PAMOJA NA KUENDELEA KUIMARIKA KWA FURSA ZA AJIRA.
"KWA UJUMLA MCHANGO WA KIA KATIKA UCHUMI WA TANZANIA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 KUTOKANA NA AJIRA ZA KUDUMU 3264 AMBAZO KUTOKA TASNIA MBALIMBALI ZINAZOHUSIANA NA UENDESHAJI WA KIA ZIKO PALE,WATU WANAFANYA SHUGHULI TOFAUTI PALE UWANJANI KUSISIMUA UCHUMI WA KANDA YA KASKAZINI,KUWAWEZESHA KUKUA KWA SEKTA NYINGINE MTAMBUKA,USAFIRI WA ANGA NI CHACHU KUWAWEZESHA KUKUA KWA SEKTA NYINGINE MTAMBUKA IKIWEMO SEKTA YA UTALII,MIFUGO NILIVYOZUNGUMZA NYAMA ZINAPITA PALE,KILIMO,MBOGA,MATUNDA NA MAUA NA BIASHARA AMBAPO HUIMARISHA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIUCHUMI KUPITIA MNYORORO WA THAMANI TUNAOTOKA NA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA KIA.
0 comments:
Chapisha Maoni