Wavamizi hao waliokuwa na silaha waliwajeruhi pia watu kadhaa wakati wa shambulio hilo katika bunge la taifa la Libya huko Tripoli. Hayo yameelezwa na msemaji wa Bunge Omar Hmeidan. Wavamizi hao wanasadikiwa kuwa na uhusiano na wagombea waliobwagwa katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha Waziri Mkuu wa Libya
Hata hivyo shambulio hilo dhidi ya bunge la taifa la Libya lilimalizika mara moja, na kuwalazimisha wabunge kuakhirisha kupiga kura ya kumchagua Waziri Mkuu Mpya hadi wiki ijayo.
0 comments:
Chapisha Maoni