| Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu |
Dodoma. Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema),
Tundu Lissu jana amewalipua baadhi ya mawaziri na wabunge kwa kugeuka ombaomba
katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
Akizungumza bungeni jana katika mjadala wa bajeti ya Wizara
ya Kazi na Ajira kwa mwaka 2014/15, Lissu alisema kuwa atawasilisha hoja
binafsi katika Ofisi ya Spika ili iundwe tume kwa ajili ya kuwachunguza wabunge
na mawaziri hao.
Huku akionyesha baadhi ya nyaraka ambazo wabunge hao
wameiandikia mifuko hiyo ya jamii kuomba fedha, Lissu alisema kitendo hicho
kimewafanya viongozi hao kusifia kila jambo linalofanywa na mifuko hiyo, hata
kama ni baya.
Lissu alitoa kauli hiyo huku wabunge watano kati ya wanane
waliomtangulia kuchangia mjadala huo, kuisifia mifuko ya hifadhi ya jamii
nchini, huku wakimtaja kwa jina Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Ramadhan Dau kwamba ni mfano wa kuigwa.
“Sifa hizi zina sababu yake. Kuna nyaraka na barua
zinazoonyesha wabunge mbalimbali waliochukua fedha za mifuko hii kwa sababu
mbalimbali,” alisema Lissu na kuongeza;
“Naomba baadaye Bunge liunde kamati teule ili kuichunguza
mifuko hii na viongozi hawa.”
Hata hivyo, Lissu hakumalizia hoja yake hiyo baada ya muda
wake wa kuchangia kumalizika na kutakiwa kukaa chini na Mwenyekiti wa Bunge,
Mussa Azzan Zungu.
Wahusika
Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho cha Bunge, Lissu
alilionyesha gazeti hili nyaraka za vigogo hao zikionyesha wote wameomba kati
ya Sh500,000 hadi Sh10 milioni.
Kati yao wapo mawaziri, naibu mawaziri ambao wameomba fedha
hizo kwa ajili ya matumizi mbalimbali, huku baadhi yao wakieleza kuwa fedha
hizo ni kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo katika majimbo yao, ikiwa
pamoja na kununua jezi na mipira.
Sakata hilo pia linaihusisha Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo kigogo mmoja wa wizara hiyo (jina tunalo)
ameomba mfuko mmoja wa jamii kumnunulia vifaa vya ofisi ikiwamo kompyuta kwa
ajili ya matumizi ya wizara.
“Unaweza ukajiuliza maswali mengi. Wizara inaomba fedha
katika mfuko wa jamii ili kununua kompyuta na vifaa vingine vya ofisi wakati
ina bajeti ya ununuaji wa vifaa hivyo.
About Dira Ya Maisha
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Chapisha Maoni