Shirika
la afya duniani WHO limesema kwamba kuenea kwa ugonjwa wa Ebola nchini
Liberia pengine kumepunguzwa kwa kiasi kikubwa,lakini ni mapema mno
kusemba kwamba ugonjwa huo umedhibitiwa.
Kaimu mkurugenzi wa
WHO,Bruce Ayward,aliwaambia waandishi habari kuwa idadi ya
walioambukizwa uko wa Ebola iko palele haijaonhezeka,na maziko
yamepungua.Bwana Aylward amesema kwamba anaimani kuwa mapambano ya ugonjwa wa Ebola na virusi vyake sasa unaelekea kudhibitiwa.
Lakini ameeleza kuwa wataalamu wa Afya wanafuatilia kwa ukaribu mno kama kuna ongezeko lolote la idadi ya wagonjwa na vifo vipya, na kuonya kwamba ishara hiyo ndogo ya matumaini haina maana kwamba ugonjwa umedhibitiwa na haupo lah hasha.
0 comments:
Chapisha Maoni