Waziri mkuu wa Uturuki, Binali Yildirim, sasa anasema kwamba Uturuki ina nia ya kujenga na kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi jirani Syria.
Katika hatua hiyo ya hivi punde na ya kushangaza, Uturuki inasema nia hasa ni kujaribu kuboresha uhusiano bora na majirani wake.
Hii inazua picha tofauti kwani Uturuki imekuwa ikishinikiza kung'atuliwa uongozini kwa rais wa Syria Bashar al-Assad.
Vyombo vya habari katika maeneo hayo yanasema kuwa wanadiplomasia wa Uturuki na Syria wamefanya mazungumzo kadhaa katika siku za hivi karibuni.
Katika majuma ya hivi karibuni, Uturuki imemaliza uhasama na Israel pamoja na Urusi na kujenga upya uhusiano wao.
Uturuki ilikuwa imejipata pabaya kidiplomasia na Urusi ilipofyatua moja ya ndege zake za kivita iliyokuwa ikishika doria katika mpaka wake na nchi hiyo.
Majuzi hata hivyo kiongozi wa Uturuki aliomba msamaha hadharani kwa tukio hilo lililosababisha kifo cha rubani mmoja.
Urusi ililipiza kisasi kwa kufunga safari za raia wake kuzuru Uturuki mbali na vikwazo chungu nzima za kiuchumi.
Sekta ya Utalii nchini Uturuki imeporomoka kwani ilikuwa inategemea watalii kutoka Urusi.
0 comments:
Chapisha Maoni