.

.

MATAIFA YA AFRIKA MASHARIKI YATAKIWA KUSHIRIKIANA

Na Erick Wanjala

 Katika ukuu wake Binti Mfalme Zahra Agha Khana ameziomba mataifa ya AFRIKA Mashariki kupitia viongozi wake kutoa ushirikiano na Taasisi za Agha Khan ambazo zinatatua changamoto katika jamiii.Wito huu unajiri wakati ziara ya Bintiye Mfalme Agha Khan  Katika Ukanda wa AFRIKA Mashariki ambapo tawi zaidi za Chuo cha Agha Khan zimefunguliwa Arusha Tanzania,Kampala Uganda na Kadhaa Nairobi Kenya.

 Dr Tumbwene Mwansisya kutoka Daresalaam akiongoza msafara wa wahitimu mjini Nairobi katika Chuo kikuu Cha Agha Khan maeneo ya Parklands.

Kwenyehotuba yake aliyoitoa katika Mahafali ya 40 ya Chuo cha Agha Khan ambapo zaidi ya  wahitimu  1000 wa Shahada ,stashahada na uzamifu kutoka   Nairobi, Kampala, Daresalaam na Pakistan ,Zahra Agha Khan alieleza umuhimu wa Viongozi kuipa taasisi ya Agha Khan mazingira rafiki katika kutekeleza mipango na maaono ya Chuo Hicho ambacho kimebobea katika maswala ya elimu na Afya ."

Hii Leo tumeweza kushuhudia  wahitimu wakipata Shahada zao mbalimbali Chuo kikishirikiana na serikali za Afrika ya mashariki tutapata baadhi ya changamato jamii inakumbana nayo zinatatuliwa kwa urahisi bila ya shida yoyote hii ni iwapo Kuna uhusiano mwema "Zahra Agha Khan

Rais na naibu Chansela Sulaiman  Shahabuddin wa Chuo cha Agha Khan kwa upande wake alitaka siku hiyo kuitwa "Muda wa Kutuzwa " kwa wahitimu akitaja kuwa Chuo Hicho kimewatuza zaidi ya wahitimu 20000 wa stashahada ,Shahada na vieti maalumu kwa walio hitimu mpaka kufikia hapo Jana.Akieleza mpango kazi ya miaka Tano alieleza mipango ya Chuo katika kuanzisha programu zingine za Shahada katika sekta ya data sayansi ,elimu kwa walimu na Tatifi mbalimbali

"Chuo cha Agha Khan kimeweza kufanikisha mengi katika miongo minne yote haya ni kupitia ukuu wake Agha Khan, na kupitia maono na ushauri wake tumeweza kufanya maamuzi sahihi hasa yalihakikisha Chuo na taasisi kwa jumla kinasoge" Alisema Rais Sulaiman Shahabuddin.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni