.

.

MERU,SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKA HISTORIA YA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA ELIMU MILIONI 470 ZATOLEWA UJENZI SHULE MPYA.


Awamu ya Sita kazini

Serikali ya awamu ya sita  ikiongozwa na  Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka historia  katika Sekta ya Elimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo ilitoa Shilingi Milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Amsha katika kata ya Ambureni ambayo haijawahi kuwa na Shule ya Sekondari kwa miaka 14 toka Halmashauri ya Meru kuanzishwa Mwaka 2007.


Mwaka 2022 Serikali ya awamu ya sita imeweka  historia kwa  wanafunzi wa kidato cha kwanza kupangwa wote kwa awamu moja bila kusubiri awamu nyingine hii ni kutokana na uwepo wa madarasa na samani za kutosha ambapo Serikali ya awamu ya sita  ilitoa  Bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vipya 70 vya madarasa na samani zake (Meza na Viti)  katika shule za Sekondari 33 katika  Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Meru .


🇹🇿✍️Hakika elimu bora kwa wote tunayaishi kwa vitendo💪


Meru tunanufaika na matunda ya awamu ya 6

 *Kazi Iendelee.....*


Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni