Na Onesmo Elia Mbise
eliaonesmo@gmail.com
Mtandao wa Wadau wanaopambana na unywaji wa pombe kupita kiasi nchini Tanzania {TAAnet} umeishauri serikali kuchukuwa hatua kali ili kudhibiti matumizi ya pombe kupita kiasi kwa kuridhia uwepo wa sera ya afya yenye kuweka katazo la matumizi mabaya ya pombe ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa muongozo wa kudhibiti utengenezaji, usambazaji na matumizi ya kinywajichochote kile chenye kilevi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo hii 02 October, 2022 na katibu wa mtandao huo Bi Gladness Hemedi Munuo, imeeleza kuwa Katika kuadhimisha ya siku ya ‘KUPINGA MATUMIZI YA POMBE KUPITA KIASI ULIMWENGUNI’ (NO ALCOHOL DAY) siku ambayo huadhimishwa kila siku ya tarehe 03 Octoba ya kila mwaka Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini Tanzania, na linapaswa kudhibitiwa kwa haraka iwezekanavyo hasa wakati huu ambapo kuna aina nyingi za vilevi vyenye kileo kwa asilimia kubwa.
Vilevile Bi Gladness katika taarifa hyo ameeleza kuwa Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani iliyotolewa tarehe 9 May, 2022,Inaonyesha kuwa Matumizi mabaya ya unywaji pombe ni moja wapo ya chanzo cha magonjwa takribani 200 zikiwepo ajali za barabarani.
Bi Gladness Munuo Amehitimisha kwa kueleza kuwa taarifa hii fupi, wana inaimani kubwa Tanzania inapokumbuka siku ya ‘KUTOKUNYWA POMBE DUNIANI’ kama ilivyotolewa kwa niaba ya Mtandao wa Asasi zinazopinga matumizi mabaya ya pombe nchini Tanzania TAAnet, Serikali Itaendelea kuchukuwa hatua Zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni