.

.

TANROAD KUSIMAMIA MIRADI 43 YA UJENZI WA BARABARA HAPA NCHINI.

 Na Jackline Lendava-Dodoma.

Katika mwaka wa fedha 2021/22, kati ya Julai 2021 hadi Mei 2022, jumla ya mikataba 20 inayohusisha miradi ya ujenzi wa Barabara na Viwanja vya Ndege inayogharimiwa moja kwa moja na fedha za ndani na mingine kugharimiwa kwa fedha za Washirika wa Maendeleo ilisainiwa. 



Hayo yameelezwa na mhandisi mtendaji mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza utekelezaji wa majukumu ya wakala wa barabarani kwa mwaka wa fedha 2022/23 na kusema kuwa jumla ya miradi 43 ya barabara yenye urefu wa kilometa 2,021.04 kwa gharama ya shilingi bilioni 9.6 ipo chini ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. "

Mikataba ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya km 582.455 imesainiwa na mikataba ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege Msalato na kumalizia jengo la Kiwanja cha ndege Songwe pamoja na mizani ya Rubana ilisainiwa. Gharma ya miradi yote 20 ni Shilingi Bilioni 1,460.84" Mhandisi Mativila.



Aidha Mhandisi Mativila amesema kuwa jumla ya miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 imekamilika kati ya Aprili 2021 hadi sasa, yaani ndani kipindi cha Awamu ya Sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla ya Sh. Trilioni 1.37 ambayo ni pamoja na miradi ya barabara, miradi ya madaraja makubwa manne ambayo tayari yamekamilika, jumla ya madaraja matatu ambayo ujenzi unaendelea, miradi ya barabara ambayo ipo chini ha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na miradi ya barabara ambayo ipo katika hatua ya manunuzi.

"Barabara zilizokamilika ni kidahwe   Kasulu (km 63)  Mkoa Kigoma , Nyakanazi  Kibondo (Kabingo) (km 50) - Mkoa Kigoma, Mbinga  Mbamba Bay (km 66), Ruvuma, Njombe  Moronga Section (km 53.9), Njombe, Moronga  Makete Section (km 53.30), Njombe, Makutano  Natta (Sanzate) Section (km 50)  Mkoa wa Mara, Waso  Sale Jct Section (km 49), Arusha, Kikusya  Ipinda  Matema (39.10km), Mbeya, Chunya  Makongolosi (km 39), Mbeya na mengine ambayo wananchi wanajiomea wenyewe pia Miradi ya Madaraja Makubwa (4) iliyokamilika ni Tanzanite Bridge, Dar es Salaam, (km 1.03), Ruhuhu bridge along Kitai  Lituhi road in Ruvuma Region (m 98); Magara Bridge in Manyara region (m 84) na Mara Bridge in Mara Region (m 940)."



"Jumla  ya miradi 3 ya madaraja makubwa ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji kwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 701 ni J. P. Magufuli (Kigongo  Busisi)  km 3.2 (Mwanza), Pangani (m 520) na Kitengule (m 140) aidha miradiri ya barabara 62 ya barabara iko katika hatua mbalimbali za manunuzi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Barabara hizi zinajumuisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani pamoja na fedha kutoka kwa Washirika wa maendeleo. Jumla ya miradi 44 ya barabara yenye urefu wa kilometa 1,523 na gharama ya Shilingi Trilioni 3.8 ipo katika hatua mbali mbali ya ujenzi nchi nzima. Miradi hii inahusisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani na inayogharamiwa kupitia Washirika mbalimbali wa Maendeleo." Mhandisi Mativila 

Wakala ya barabara Tanzania ilianzishwa kwa waraka wa serikali uliotolewa kwenye gazeti la serikali Na. 293 la tarehe 25 Agosti, 2000 kwa mujibu wa sheria ya wakala wa serikali Na. 30 ya mwaka 1997 yenye majukumu ya kuratibu na kusimamia, ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara kuu na za Mikoa zenye urefu wa kilometa 36,362.


Kupima na kufanya utafiti kuhusu vifaa vya ujenzi wa barabara kupitia Kitengo cha Maabara Kuu ya Vifaa (Central Materials Laboratory) na maabara ndogo zilizopo katika kila mkoa, kudhibiti uzito wa magari barabarani na kulinda maeneo ya hifadhi ya barabara.  Kwa sasa Wakala ina mizani 70 ya kudumu, 22 ya kuhamishika na mizani 15 (Vigwaza 2; Mikese 1; Dakawa 2; Njuki 2; Nala 2; Mpemba 2; Wenda 2; Kimokouwa 2) ya kupima uzito wakati gari linatembea (Weigh in motion) na kusimamia usanifu na ujenzi wa Viwanja vya Ndege nchini.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni