.

.

Mabinti wa Mfalme Abdullah walioasi Saudia wasifiwa

Mabinti wa Mfalme Abdullah walioasi Saudia wasifiwa


 


Mwana Mfalme wa Saudi Arabia ameeleza mshikamano wake na kwamba yuko pamoja na mabinti wa Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia wambao wamewekwa chini ya kifungo cha nyumbani katika mji wa Jeddah nchini humo. Katika ujumbe alioutuma katika ukurasa wake wa Facebook, mwana mfalme Khalid bin farhan al Saud amewasifu binti mfalme Sahar na dada zake watatu kwa kuunga mkono mapambano ya raia waliodhulumiwa wa mji wa Qatif katika mkoa wa mashariki wa huko Saudi Arabia.
Mwana mfalme Farhan alijitenga na familia hiyo ya kifalme mwezi Julai mwaka jana akisema kuwa utawala wa Saudi Arabia haujasimama kwa misingi ya sheria za Mwenyezi Mungu. Mwana mfalme Khalid bin Farhan al Saud ametoa matamhsi hayo baada ya binti wa mfalme aliye na umri wa miaka 42 kuwataka wananchi wa Saudia kuendeleza maaandamano yao dhidi ya utawala wa Aal Saud. Sahar, Maha, Hala na Jawaher al Saud ni mabinti wa Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ambao inasemekana kuwa hivi sasa wako katika kifungo cha nyumbani huko Jeddah.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni