.

.

'Palestina ina haki ya kujilinda mbele ya adui Mzayuni’

'Palestina ina haki ya kujilinda mbele ya adui Mzayuni’

Mwanachama wa kamati kuu ya harakati ya Fat'h ya Palestina amesisitiza kuwa, Wapalestian wana haki ya kuendesha muqawama na kujilinda kwa nyenzo zote. 
Mahmoud al Aalul amesema kuwa, harakati za Fat'h na Hamas licha ya kuhitilifiana katika baadhi ya mambo, lakini daima zimekuwa rafiki na ndugu na kwamba adui wa siku zote wa harakati hizo ni Israel.

  Mahmoud al Aalul amesema kuwa kujilinda nafsi ni haki iliyosisitizwa katika sheria zote za kimataifa, na kwamba hatua ya kujilinda na kujitetea wanachama wa harakati ya Hamas kwa nyenzo zote na njia zinazowezekana mbele ya adui Mzayuni, ni haki yao ya wazi. Aalul amesisitiza pia kuwa Hamas na Fat'h zinaheshimu makubaliano yao ya umoja wa kitaifa na kuongeza kuwa Wazayuni hawana azma ya kweli ya kushiriki kwenye mwenendo wa mapatano bali wanachotaka wao ni kuendeleza mauaji na umwagaji damu dhidi ya raia wa Palestina na kamwe Wapalestina hawatasalimu amri mbele ya jinai hizo za Wazayuni Maghasibu. 

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni