.

.

Manowari za Iran zatia nanga Djibouti

Manowari za Iran zatia nanga Djibouti

Manowari ya IranManowari ya Iran
Msafara wa 29 wa Meli za Kivita za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimetia nanga katika Bandari ya Djibouti katika stratijia ya Iran ya kuimarisha doria katika maji ya kimataifa. Msafara huo uliowasili Djibouti Jumatatu unajumuisha Manowari wa Kharg yenye uwezi wa kusheheni helikopta na Manowari ya Ushambuliaji ya Sabalan. Msafara huo umekuwa ukilinda doria katika Bahari ya Sham, Ghuba ya Aden na eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi. Msafara huo utasalia Bandari ya Djibouti kwa muda wa siku tatu kabla ya kuelekea Bahari ya Atlantiki.
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayyari hivi karibuni alinukuliwa akisema  msafara huo uko katika maji ya kimataifa kwa lengo la kulinda meli za kibiashara za Iran na pia kutoa mafunzo kwa vijana waliojiunga na Jeshi la Wanamaji. Sayyari alisema Iran ni kati ya nchi muhimu duniani ambazo zinalinda doria katika njia za baharini zenye maharamia hasa Ghuba ya Aden na Lango la Bab al-Mandab.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) limelipongeza Jeshi la Wanamaji la Iran kwa mafanikio yake katika kupunguza uharamia baharini.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni