Siku ya hakimiliki dunia 26 Aprili yaangazia filamu na hakimiliki:WIPO
Filamu zimeendelea kuwa na mvuto duniani kote kutokana na vile zinavyojihusisha na jamii husika. Kuanzia filamu zile za kimya kimya hadi za sasa zinazotumia teknolojia ya juu bado mvuto na msisimko ni ule ule licha ya teknolojia kubadilika. Shirika la hakimiliki duniani WIPO linasema ubunifu wa waandaaji na waigizaji wa filamu umeendelea kuleta msisimko huo lakini mustakhabali wa watendaji hao uko mashakani kutokana na teknolojia za kisasa na hata ukiukwaji wa haki miliki bunifu zao. Je kivipi? Basi ungana na Assumpta Massoi wa Idhaa hii katika mahojiano yake na Neema Nyerere-Drago afisa programu mwandamizi wa WIPO ambaye anaanza kwa kuelezea maana ya hakimiliki bunifu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya hakimiliki duniani tarehe 26 mwezi Aprili.
0 comments:
Chapisha Maoni