.

.

BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO NCHINI (CPB) KUZALISHA MAFUTA NA KUNI KUPITIA PUMBA ZA MPUNGA

 Na Jackline Lendava-Dodoma.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania CPB,yaja na mpango wa kupunguza uharibifu wa Mazingira na gharama za maisha kwa wananchi kwa kuzalisha mafuta na kuni kupitia pumba za mpunga.


Ameyaeleza haya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko CPB, Dkt. Anselm Moshi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma.



Dkt. Moshi amesema kwasasa wapo katika upembuzi yakinifu ili kuongeza thamani ya zao la mpunga ili kuweza kuzalisha mafuta yatokanayo na pumba za mpunga.na kuongeza kuwa CPB imedhamiria kuwafikia wakulima wengi zaidi ili wazalishe kwa ufanisi shambani.


"Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko CPB dhamira yake ni kuwawezesha wakulima kulima kwa kutumia mbinu za kisasa kwa maslahi yao binafsi na Taifa kwa ujumla"


"Pia tunampango wa kuanza kutumia teknolojia ya kuzalisha mafuta ya kupikia yatokanayo na pumba za mpunga kupitia kiwanda chetu kilichopo Mkuyuni jijini Mwanza"


Aidha,amesema kuwa kwa Mwaka 2021/2022 wamenunua mazao Tani Elfu 26,665 yenye Thamani ya shillingi Bilion 14.8 na kuongeza Thamani mazao Tani elfu 16.3 yenye Thamani Bilion 8.2.


Dkt. Moshi amesema kuwa ili mkulima apate mapato mengi anatakiwa kulima kwa Tija na kuendana na soko la kibiashara.


"Ikumbukwe kuwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko CPB, ni Taasisi ya serikali chini ya wizara ya Kilimo iliyopewa dhamana ya kufanya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko na imeanzishwa kwa sheria ya nafaka na mazao changanyiko Namba 19 ambapo pia hadi sasa mzunguko wa biashara katika taasisi hiyo umeongezeka kutoka bilioni 15 hadi bilioni 52,"

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni