.

.

RAIS SAMIA AIWEZESHA TUME YA UTUMISHI WA WAALIMU NCHINI.

Na Jackline Lendava-Dodoma

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, ameiwezesha Tume ya utumishi wa walimu  Katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi, 2021 hadi mwezi Septemba, 2022, kutekeleza majukumu mbalimbali ambayo yameendelea kuboresha mazingira ya Walimu na Sekta ya Elimu kwa ujumla ambayo ni Ajira na Maendeleo ya Walimu.



Hayo yameelezwa hii leo Oktoba 27,2022 na katibu mtendaji wa tume ya utumishi wa walimu Mwl. Paulina Nkwama wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa kwa  kila Mwalimu aliyestahili kupandishwa  cheo na zoezi hilo ni endelevu.



"Walimu  16,749  wakiwemo 8,949 wa Shule za Msingi na 7,800wa Shule za Sekondari, jumla ya Walimu 15,802 walisajiliwa, Walimu wa Shule za Msingi walikuwa 8,512na Sekondari walikuwa 7,290, Walimu 6,949 kwa sawa na asilimia 100 walithibitishwa kazini wakiwemo 3,949 wa Shule za Msingi na 3,000 wa Shule za Sekondari jumla ya Walimu 47,158 walipandishwa cheo (Walimu 22,943 ni wa Shule za Msingi na 11,524 wa Sekondari kwa mwaka 2021/2022). Aidha kwa mwaka 2020/2021 walimu walipandishwa cheo ni 126,346. Walimu 12,546 walibadilishiwa vyeo baada ya kujiendeleza kielimu, kati ya hao Walimu 9,059 ni wa Shule za Msingi na Walimu 3,487 ni wa Shule za Sekondari. katika kipindi hicho jumla ya Walimu 3,912 walistaafu kazi ambapo Walimu wa Shule za Msingi walikuwa ni 3,580, kati ya idadi hiyo, Walimu 2,313 walistaafu kwa lazima 1,258 kwa hiari na tisa (9) walistaafu kwa matatizo ya afya (Ugonjwa). 

Vilevile, Walimu wa Shule za Sekondari waliostaafu ni 332 ambapo kati ya hao, Walimu 228 walistaafu kwa lazima 104 kwa hiari, walimu waliofariki ni 723 kati ya hao Walimu 521 ni wa Msingi na 202 wa Sekondari. Mkataba wa Ajira za Walimu uliokuwa umeandikwa kwa lugha ya kiingereza ulitafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ili kuwarahisishia walimu kwenye matumizi ya Mkataba huo" Mwl. Paulina.

Aidha kwa upande mwingine amezungumzia maadili ya walimu wawapo kazini ambapo amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 hadi Septemba, 2022, Tume ya Utumishi wa Walimu Makao Makuu ilitoa uamuzi wa jumla ya Rufaa 253 zilizopinga uamuzi uliotolewa na Mamlaka ya Nidhamu (Tume Ngazi ya Wilaya), na katika hizo Rufaa 152 zilizoamuliwa sawa na asilimia 61.6 zilikatataliwa na kuthibitisha adhabu iliyotolewa na TSC Wilaya (Rufaa 108 zilikataliwa na Rufaa 44 sawa na asilimia 17.4 zilitupiliwa mbali kwa kuwa ziliwasilishwa nje ya muda), Rufaa 53 sawa na asilimia 20.9  zilikubaliwa, na Rufaa 48 sawa asilimia 18.9 zilirejeshwa kwenye Mamlaka ya Nidhamu kuanza upya kutokana na kufikia uamuzi bila kuzingatia ipasavyo taratibu za uendeshaji wa mashauri.

Ameongeza kuwa katika kipindi hicho tume ya utumishi ya walimu makao Makuu ilipokea nakala ya rufaa 64 zilizokatwa kwa Rais kupinga uamuzi wa Tume na tume iliandaa mwenendo na vielelezo vya rufaa 56 na kuwasilisha kwa Rais, Aidha, Tume inaendelea kuandaa mwenendo na uchambuzi wa rufaa 8 zilizobaki kwa hatua ya kuwasilishwa.

"Kamati ya nidhamu inatekeleza majukumu yake kwa haki na usawa bila kubagua, kosa lolote atakalofanya mwalimu na likadhibitika kwa sababu unaweza ukazushiwa pia kwamba mwalimu amefanya kosa kumbe ni kwa sababu yupo makini katika kazi yake, hata ukiwa na mahusiano na mwalimu mwezio bila utaratibu yaani utaratibu usioeleweka ni kosa la kinidhamu, mwalimu atapewa hati ya mashitaka na kujieleza akisema anaonewa itaundwa kamati, itaita mashahidi pande mbili na vielelezo vya kuthibitisha hilo baada ya hapo sheria itaamua" Mwl Paulina.

Mwl. Paulina amesema kuwa katika tume ya Utumishi wa Walimu kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/23 imeweka vipaumbele vya kusimamia Utumishi na Maendeleo ya Walimu kwa kudumisha Maadili na Nidhamu kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Utumishi wa Umma, kuhakikisha kwamba Walimu wenye sifa ya kupandishwa vyeo na kubadilishiwa kazi wanapata huduma hiyo kwa wakati baada ya kibali kutolewa na Mamlaka husika.

  Aidha  ameeleza kuwa kipau mbele kingine ni kuendelea na ujenzi wa Jengo la Ofisi za Tume Makao Maku, Kufuatilia Ukamilishaji wa Muundo wa Maendeleo ya Utumishi na Mishahara wa Tume, kuanza kutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Masuala ya Utumishi wa Walimu kwa majaribio na kuendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa Mfumo huo kuanzia ngazi ya Shule kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi wa Tume kwa kuwaongezea ujuzi, kuwapatia ofisi na vitendea kazi na kuongeza uelewa kwa Wadau kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu na majukumu yake.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni