.

.

WAKALA WA TAIFA WA CHAKULA NCHINI HUTOA ZAIDI YA AJIRA 3000.

 eliaonesmo@gmail.com

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Tanzania (NFRA) hutoa ajira zaidi ya 3,000 za muda mfupi zinazochangia kuongeza kipato kwa wananchi.


Haya yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA, CPA Milton Lupa katika Taarifa yake ya Utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita aliyoitoa Jijini Dodoma.



"NFRA imefanikiwa kuongeza fursa za kiuchumi kwa sekta mbalimbali kupitia kazi za usafirishaji,ununuzi wa vifaa mbalimbali vya uhifadhi na viuatilifu. Aidha NFRA hutoa ajira za muda mfupi kwa wananchi zaidi ya 3,000 zinazochangia kuongeza kipato kwa wananchi. Ajira hizo zinazotokana na kazi mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi la ununuzi wa nafaka,uhifadhi na kipindi cha uzungushaji wa nafaka na utekelezaji wa Mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka"


Aidha NFRA unatekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka,ambapo ukikamilika utaongeza uwezo wa kuhifadhi kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000.



Ambapo CPA Lupa ameeleza kuwa NFRA imefanikiwa kukamilisha sehemu ya Mradi na kuongeza uwezo wa kuhifadhi tani 90,000 katika kanda za Arusha (Halmashauri ya Babati) na Sumbawanga na Mpanda.



"Kukamilika kwa Mradi huo kumeongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 251,000 hadi tani 341,000 na utekelezaji wa Mradi katika maeneo mengine Dodoma, Songea,Shinyanga,Songwe na Makambako umefika asilimia 85"


Pia amesema ili kukabiliana na makali ya mfumuko wa bei za nafaka Wakala kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo imeongeza upatikanaji wa nafaka katika masoko ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi.


"Kwa kuanzia,Wakala unahudumia Halmashauri za Bunda,Sengerema,Geita, Nzega,Liwale,Nachingwea,Longido,Loliondo na Monduli ambapo takriban tani 3,000 zimepelekwa katika maeneo hayo"



Mtendaji huyo amesema kuwa Wakala imejipanga kuhudumia maeneo mengine yatakayothibitika kuwa na mahitaji ya dharura au upungufu wa Chakula.


Ametoa wito kwa wananchi kujihakikishia usalama wa chakula kuanzia ngazi ya Kaya,wahifadhi akiba ya kutosha ya chakula kipindi cha mavuno na kuuza chakula pale wanapokuwa na ziada katika uzalishaji.


Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na.30 ya mwaka 1997 na ilianza kazi rasmi julai 1,2008 ikiwa na jukumu la kuhakikishia nchi usalama wa chakula kwa kununua na kuhifadhi akiba ya chakula na kutoa chakula cha msaada kwa waathirika waliokumbwa na majanga mbalimbali ya kitaifa.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni