.

.

TULITARAJIA HAYA KWENYE MCHAKATO WA KATIBA MPYA

 Wakati Bunge Maalumu la Katiba likiendelea mkoani Dodoma, Watanzania wamekuwa wakiendelea kutoa maoni yao kwa lengo la kuuboresha na kueleza matarajio yao.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Emmanuel Kilatu ni mmoja wa Watanzania wenye mengi ya kueleza kuhusu matarajio yao katika mchakato huo.
Mbali na kupongeza kazi iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Kilatu anamwelezea Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, kuwa ni mtu makini na muadilifu, hivyo kumtuhumu kuwa amechakachua maoni ya wananchi katika Rasimu ni kukosa uungwana.
Anashauri kuwa mvutano kati ya wanaounga mkono rasimu hiyo, hasa kuhusu Muundo wa Serikali tatu na wanaoipinga wakitaka muundo wenye serikali mbili, kutumia busara zaidi.
“Sijui kwa nini viongozi wanajisahau na kudhani tunaoongozwa hatuelewi? Ukifuatilia jitihada za kutatua kero za Muungano ni dhahiri kuna umuhimu wa kuzingatia sauti ya wananchi juu ya wanachotaka,” anaeleza Kilatu.
Anarejea matokeo ya kazi zilizofanywa na tume mbalimbali, zikiwamo za Jaji Robert Kisanga na Jaji Fransis Nyalali, ambazo pia zilipendekeza Mabadiliko ya Muundo wa Muungano kutoka serikali mbili kuwa serikali tatu.
Mtazamo wa msomi huyo unaelekeza kuwa misimamo ya vyama vya kisiasa ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, haitaleta matokeo mazuri na hivyo anashauri matakwa ya watu hata kama ni wachache yazingatiwe.
Anaamini dhima ya Rasimu ya Warioba isipoharibiwa kwa ushabiki wa kisiasa, Katiba Mpya itanufaisha mtu mmoja mmoja na taifa. Manufaa hayo anayaelezea katika nyanja za elimu na siasa.
Elimu
Kilatu ambaye ni mwalimu kitaaluma. Anasema hali ya elimu nchini ni mbaya na kiini chake ni kukosekana kwa msimamo wa kitaaluma katika mambo yanayohusu Sekta ya Elimu.
“Watu kwa kutumia kigezo cha ‘utaalamu’ wanajifungia mahala na kuingiza mambo ya kitaaluma yasiyotekelezeka kwenye mitalaa. Hayo ni matokeo ya kuwa na Katiba isiyokidhi matakwa ya jamii katika utumishi wa umma,” analeza Kilatu.
Kilatu anashauri wanaoboresha rasimu ili kupata Katiba itakayopendekezwa wakumbuke hawatabaki madarakani milele.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni