.

.

Bodi ya filamu Nchini Tanzania imeunda kamati maalum ya kurudisha ule utamaduni wa kutazama filamu katika kumbi za sinema.

 Na Deborah Lemmubi-DODOMA.

Bodi ya filamu Nchini Tanzania imeunda kamati maalum ya kurudisha ule utamaduni wa kutazama filamu katika kumbi za sinema.

Hayo yamesemwa na Katibu mtendaji wa Bodi ya filamu Nchini Dkt Kiagho Kilonzo katika mkutano wake na vyombo vya habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo katika ukumbi wa idara habari Maelezo Jijini Dodoma.

"Bodi imeunda Kamati maalum ya kurudisha utamaduni wa kutazama filamu katika Kumbi za Sinema. Hatua hiyo inatarajiwa pia kutoa mchango stahiki katika uchumi wa wadau wa Sekta na Taifa kupitia viingilio vya mlangoni. 

 Katibu mtendaji wa Bodi ya filamu Nchini Dkt Kiagho Kilonzo


Kwa upande wa usambazaji Serikali ina makubaliano na kimataifa Televisheni Mtando ya Nuella (Nuella Online TV) ya nchini Uholanzi kununua na kuonesha Filamu za Kitanzania, na hadi sasa kuna filamu tisa (9) zinaonyeshwa huko". 

Aidha Dkt Kilonzo amezungumzia suala la Bodi kupigania haki na maslahi ya wasanii nchini.

"Kusimamia Haki na Maslahi ya Wasanii 

Bodi ya Filamu inaratibu Kamati Maalum ya kutetea Haki za Wasanii iliyoundwa na Waziri mwenye dhamana ya kusimamia maswala ya Sanaa nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na kuhuishwa tena 2019 na 2020 (ikiwa na mabadiliko ya baadhi ya wajumbe) itakayodumu hadi mwishoni mwa mwaka 2022. Hadi sasa Kamati imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, ambapo takriban shilingi milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii:

- Malalamiko 22 yamesuluhishwa, na 

- Malalamiko 8 yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa. 

Baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa na kushughulikiwa ni yale ya marehemu Amri Athumani (King Majuto), marehemu Steven Kanumba, msani David Ganzi (Young Dee), Mzalishaji wa Tamthilya Samwel Isike, na wengineo".

Pia amesema Bodi ya filamu inalengo la kuanda fulau za kimkakati hasa za muasisi wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere na wote waliofanya mambo makubwa kwa Taifa letu.

" Filamu za Kimkakati

Program hii ina lengo la kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia (maeneo mahsusi) ya nchi kwa lengo la kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali waliyonayo. Programu hii itasaidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa kuhusisha taarifa za viongozi wetu mbalimbali waliofanya mambo makubwa kama vile Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye alisaidia ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika".

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji mkuu wa Serikali Bwana Gerson Msigwa ametumia fursa hii kuwakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi kuja kuwekeza katika kiwanda cha filamu hapa Nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji mkuu wa Serikali Bwana Gerson Msigwa .

Dira ya Bodi ya filamu ni kuwa na tasnia yenye filamu shindani kwa maendeleo ya Taifa na kupunguza umaskini.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni