.

.

CHANJO YA COVID-19 HAINA MADHARA YEYOTE KWA VIJANA.

eliaonesmo@gmail.com.

 Na Deborah Lemmubi-Dodoma

Imeelezwa kuwa kundi linalotakiwa kutiliwa mkazo katika uhamasishaji wa chanjo ya Covid19 kwa sasa ni kundi la Vijana kwani wamekuwa na imani potofu juu ya chanjo hizi kwamba wanaweza kukosa nguvu za kiume au kushindwa kuzaa kabisa mara watakapochanja.

Haya yamesemwa na Bi Flora Kimaro ambaye ni Mratibu Msaidizi wa chanjo Jiji la Dodoma,wakati akifunga mafunzo ya watendaji wa kata,wa mitaa,Viongozi wa Dini na Wataalam wa Afya yaliyolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia vyombo vya Habari katika kuelimisha jamii juu ya kujikinga na Uviko sambamba na kupata chanjo ya Uviko19,yaliyofanyika Jijini Dodoma.

"Kundi la kuhasisha sana kwa sasa ni kundi la vijana kwani wamekuwa na imani potofu juu ya hizi chanjo kwa kusema wanaweza kosa nguvu za kiume au hata kutokuzaa kabisa".

Aidha Bi Flora amesema kuwa mwenendo wa utoaji wa chanjo kwa Jiji la Dodoma unaendelea na mpaka sasa kuna vituo vya Afya vinavyotoa huduma za chanjo 65 vikiwemo vituo vinavyotembea.

"Mwenendo wa utoaji wa chanjo kwa Jiji la Dodoma,tuna vituo 65 vya Afya vikiwemo vinavyotembea na vinaendelea kutoa huduma za chanjo wilaya ya Dodoma mjini".

Pia Mratibu msaidizi amesema mpaka sasa Tanzania bado hakuna mamlaka yeyote ya Afya iliyothibitisha kutokuwepo kwa ugonjwa wa Uviko19 hivyo watu waendelee kuchukua tahadhali kama kawaida.

"Kwa Tanzania bado hatujathibisha kuwa ugonjwa wa Uviko haupo,bado wataalamu hawajasema chochote hivyo tuendelee kuchukua tahadhali kama kwa kunawa mikono na kuvaa barakoa".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mafunzo haya Shehe Musa Kalasa amesema yeye alichanja kwa utata sana kwani aliamini akichanja damu itaganda kama watu wanavyosema,lakini baada ya kupata elimu alichanja na hakupata shida yeyote.

Naye Bi Jane Shemndolwa Afisa mtendaji Halmashauri ya Mpwapwa kata ya Chitemo amesema alikuwa haamini kuhusu chanjo kutokana na maneno ya watu kuwa ukichanja chanjo ya Uviko19 unakuwa Zombi.

Juvenary Tailo aliyemwakilisha Mchungaji wa Kanisani MRB Prophetic Ministries amesema yeye alijua chanjo ni mpango wa kishetani wa kupunguza watu lakini baada ya kuhudhuria mafunzo haya amepata elimu na ameona mambo haya hayahusiani na chanjo.

Mafunzo haya yamekusanya watu mbalimbali akiwemo Viongozi wa dini ili kupata uelewa wa pamoja na wao kwenda kutoa elimu kwa jamii zao.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni