eliaonesmo@gmail.com
Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
Serikali imetenga shilingi Bilioni 22 katika mwaka wa fedha 2022/2023 ili kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ununuzi wa mitambo na vifaa vya kisasa vya Kimaabara.
Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelis Mafumiko akizungumza na wanahabari na kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali 2021/2023 iiyofanyika Jijini Dodoma.
"Ili kuendelea kuboresha na kusogeza huduma zake karibu na wananchi katika mwaka wa fedha 2022/2023,Serikali kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na mambo mengine imepanga kukamilisha utekelezaji huo wa ujenzi na ununuzi wa mitambo na vifaa vya kisasa vya kimaabara,Serikali imetenga jumla ya Shilingi 22 kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Pia kununua mitambo na vifaa vya kisasa kwaajili ya kuendelea kuboresha uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara kwa lengo la kusimikwa kwenye jengo la Mamlaka Makao makuu ya Nchi-Dodoma".
Aidha Dkt Mafumiko ameeleza azima ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani ya kuhimiza Serikali kuhamia Makao Makuu Dodoma.
"Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali chini uongozi wa Mhe Samia Suluhu Hassani Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhimiza azima yake ya Serikali kuhamia makao makuu ya Nchi Dodoma imeiwezesha Taasisi yetu kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi na Maabara lenye thamani Bilioni 8.14 eneo la Medeli Jijini Dodoma. Jengo hilo ndipo yalipo makao makuu ya mamlaka ya Maabara Mkemia Mkuu wa Serikali kwa sasa".
Pia amezungumzia suala la kuendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma zao.
"Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Mamlaka itaendelea kuimarisha zaidi matumizi ya Tehama katika utekelezaji majukumu yake ikiwa ni pamoja na kukamilisha na kuanza kutumia mfumo wa usimamizi wa Maabara,kuendelea kutumika kwa mfumo wa Serikali wa kukusanya mapato,kuendelea kutumia mfumo wa pamoja wa ugomboaji wa mizigo Bandarini na kuendelea kutumia mfum wa Bajeti".
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilianzishwa kwa Sheria Na 8 ya mwaka 2016 na kupewa wajibu wa kutekeleza Uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara wa Sampuli na Vielelezo,Utoaji wa ushahidi Mahakamani na Usimamizi na uthibiti wa kemikali za Viwandani na Majumbani.
Kazi nzuri
JibuFuta