.

.

NCHI HAITAKUWA NA UHABA WA SUKARI KWA MIAKA MIWILI IJAYO

eliaonesmo@gmail.com

Na Deborah  Lemmubi -Dodoma.

 Bodi ya Sukari Tanzania imesema kuwa Nchi haitakuwa na uhaba wa sukari kwa kipindi Cha Miaka miwili ijayo kwani uzalishaji utaongezeka kutoka Tani 380,000 za Sasa hadi kufikia Tani 756,000 ifikipo Mwaka 2025/2026.



Uhaba wa Sukari utaisha katika kipindi hicho kutokana na Mikakati mbalimbali iliyowekwa na bodi hiyo kwa kuongeza viwanda vya ndani.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania,Prof.Kenneth Bengesi katika mkutano wake na wana habari Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.


Prof.Bengesi ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia suluhu hassan imedhamiria kuongeza uzalishaji wa sukari nchini kwa kujenga viwanda vingi ili kuongeza ajira kwa Watanzania. Na  kubainisha kuwa kwa sasa Serikali inatumia fedha nyingi kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ambapo serikali inatumia zaidi ya dolla million 150 ambazo ni zaidi ya billion 300.


"Serikali inatumia zaidi ya dolla million 150 ambazo ni zaidi ya billion 300 kuagiza sukari nje ya nchi jambo ambalo linawezekana kuzuilika endapo tutadhamiria kwa pamoja kuongeza uzalishaji wa sukari nchini kwa kujenga viwanda vingi jambo ambalo pia litaongeza ajira kwa Watanzania"


 "sisi kama chombo cha udhibiti chenye ufanisi na kinachoweza kuhudumia na kusaidia tasnia ya sukari kufikia ushindani na uendelevu unaotakiwa tuna jukumu la kuisaidia serikali kupunguza gharama za uagizaji wa Sukari kutoka nje na ili tufanikiwe ni lazima tuwekeze kwenye ujenzi wa viwanda"



 Bodi ya Sukari Tanzania kwa kuongozwa na kanuni za kutoa huduma kwa usawa, ubora na uadilifu, inalenga kuunda, kudumisha na kudhibiti mazingira ambayo yanawafaa wawekezaji wa sukari kuzalisha miwa, sukari na bidhaa zinazohusiana kwa ufanisi na kwa faida.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni