.

.

RAIS SAMIA KUTANGAZA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI.

 eliaonesmo@gmail.com

 Na Deborah Lemmubi-Dodoma

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 tarehe 31 Oktoba, 2022 katika uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma.



Akitoa taarifa hii kwa Umma kupitia Vyombo habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule amesema kuwa Maandalizi ya uzinduzi huo yanaendelea vizuri na Serikali imejiandaa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata fursa kufahamu matokeo ya Sensa.


Senyamule amesema kwa mujibu wa Mpango wa Utekelezaji na Usimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu, kazi zinazotakiwa kufanyika ni kuchakata taarifa zilizokusanywa ili kupata matokeo yake na hatimae kutangazwa rasmi kwa umma matokeo ya mwanzo.


"Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu tarehe 5 Septemba, 2022 wataalamu wetu walianza zoezi hilo la uchakataji wa taarifa. Hadi sasa matokeo ya mwanzo yako tayari kwa uzinduzi,"Amesema Senyamule


Na Kuongeza kuwa "Ninayo furaha kutangaza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan atazindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 tarehe 31 Oktoba, 2022 katika uwanja wa michezo wa Jamhuri jijini Dodoma,"Senyamule


Mkuu wa Mkoa ametolea mifano kwa Sensa zilizopita ikiwemo ile ya mwaka 2002na 2012 ambazo zilitumia teknolojia ya usomaji wa vivuli (Scanning Technology), matokeo ya Sensa hizo yalizinduliwa rasmi miezi mitatu baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu ,wakati Sensa ya mwaka 2022 matokeo yake yanazinduliwa mwezi mmoja baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu na makazi.


"Kwa Sensa ya mwaka huu, matokeo yake kama mnavyoona yatatoka ndani ya kipindi cha mwezi mmoja baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu ,ambapo ni mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Sensa nchini kwetu na yamewezekana kutokana na matumizi makubwa ya tekinolojia za kisasa hasa matumizi ya vishikwambi katika awamu zote za utekelezaji wake na utashi wa Siasa katika kusimamia zoezi hilo kuanzia maandalizi hadi leo," Amesema Senyamule


Wakati huohuo RC Senyamule ametumia nafasi hiyo kupitia vyombo vya habari kutoa wito kwa wananchi wote Mkoa wa Dodoma, Taasisi zote, Watumishi wa Umma wote na wa Sekta binafsi Mkoani Dodoma, Makundi mbalimbali katika jamii (wafanya biashara, Dini, Walemavu, Bodaboda, Machinga, Wazee n.k) na wananchi kutoka Mikoa yote jirani kumuenzi Rais kwa kujitokeza kwa wingi tarehe 31 Oktoba, 2022 kwenye viwanja vya Jamhuri kujumuika katika katika tukio hilo.


Ikumbukwe kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikamilisha rasmi zoezi la Kuhesabu Watu, Kuhesabu Majengo, na Kuhesabu Anwani za Makazi kupitia mfumo wa utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 tarehe 05 Septemba, 2022.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni