NA SALMA SEFU,
KILIMANJARO
Miti takribani 2500 hadi sasa imefanikiwa kupandwa katika maeneo mbali mbali ya vyanzo vya maji Mkoani Kilimanjaro lengo ni kufika Asilimia 85-90 ifikapo january huku adhma ya kampeni hii ya upandaji miti ikiwa ni kupanda miti Milioni moja na laki tano Nchi nzima.
Katika Mkoa wa Kilimanjaro Kampeni hii ya upandaji miti imezinduliwa rasmi hii leo na mwenyekiti Mratibu wa zoezi la upandaji miti Bw. Agustino Matefu katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro KI NAPA huku vijana wa Seneti Mkoa wa Kilimanjaro wakishiriki katika zoezi la upandaji miti katika moja ya chanzo cha maji kilichopo hifadhini hapo.
Aidha Bw. Agustino Matefu-mwenyekiti mratibu kampeni ya upandaji miti amesema
kampeni hii ya upandaji miti imehusisha vijana kwa lengo la kuleta hamasa katika Nchi kwani vijana wana wajibu wa kurithishwa kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji.
Tunajua nguvu gani ya vijana katika Nchi inaweza kuleta mabadiliko chanya tunaweza kuandaa kizazi kijacho chenye desturi na tabia ya kutunza vyanzo vya maji katika Nchi,Tumeona katika baadhi ya hifadhi kama Ruwaha wanyama wanateseka kwenda hadi Kenya kutafuta maji hivyo sisi kama vijana tupo tiari kushirikiana na mamlaka zote ambazo zipotiari kuhakikisha kwamba mazingira katika Nchi yetu yanapewa kipaumbele .Tunahakikisha tunakwenda kuimarisha vyanzo vyetu vya maji Nchi nzima kila kwenye maporomoko panapo hitaji kupandwa miti tutapanda miti ya Asili''Bw. Agustino Matefu''
Hata hivyo Afisa Mhifadhi msaidizi mwandamizi Bi.Zawadi Mahinda amesema licha ya jitihada za upandaji wa miti bado wanatoa elimu ya Uhifadhi kwa wananchi kwa vijiji takriban 94 vinavyozunguka hifadhi.
Tunataka wananchi wajue manufaa ya uhifadhi,pasipo elimu ya uhifadhi wananchi watakuwa wagumu kuelewa pindi tutakapotoa onyo la uharibifu wa mazingira katika hifadhi,. hivyo tunajaribu kushirikiana nao ili waweze kutambua umuhimu wa hifadhi yetu na washiriki katika kulinda maeneo haya kwa manufaa yao binafsi kwani tumekuwa tukigawa miche ya miti ya asili pia katika vijiji hivyo 94 waweze kupanda na kuvuna pindi inapokuwa kuepusha ukatwaji wa kuni na mbao ndani ya hifadhi.Bi.Zawadi Mahinda''.
0 comments:
Chapisha Maoni