KILIMANJARO
SALMA SEF
Wafugaji wa nyuki katika hifadhi ya msitu wa West Kilimanjaro wilayani siha Mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuwawezesha mitaji ili waweze kuongeza mizinga ya nyuki itakayowasaidia kuongeza uzalishaji wa asali.
Wakiwa katika shughuli zao za kila siku katika shamba la miti la West Kilimanjaro hii leo wafugaji hawa wa nyuki wanasema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni uchache wa mizinga jambo linalorudisha nyuma uzalishaji wa asali.
Mmoja wa wanakikundi kinachojihusisha na ufugaji wa nyuki katika shamba la miti la Westi Kilimanjaro anaefahamika kwa jina la Julius Mbananje amesema ufugaji wa nyuki katika shamba hilo unawasaidia kujikwamua kiuchumi licha ya kuwa bado hawajaweza kusimama imara kulingana na changamoto kadha wa kadha zinazo wakabili ikiwemo kukosa mizinga ya kutosha itakayo wawezesha kurina asali kwa wingi.
"Kiukweli tuna nufaika sana na shamba la miti la West Kilimanjaro,Unajua katika umri wangu ni vigumu sana kufanya kazi ngumu ila ufugaji wa nyuki unanirahisishia sana maisha,.Naweza kutumia muda mfupi sana shambani nikihudumia mizinga yetu ya nyuki lakini kwa manufaa makubwa sana ya baadae kwani faida ni kubwa kuliko muda ninaotumia kama mzee.,Mzinga mmoja wa nyuki unauwezo wa kutoa kilo saba ya Asali hivyo utaona ni jinsi gani ufugaji wa nyuki unaweza kusaidia kuondokana na janga la umasikini.
Changamoto ni kwamba hatuna mizinga ya kutosha kulingana na uhitaji wa soko letu,tunavuna asali chache naomba serikali na wadau waliangalie hili kwani hii ndio ajira yetu sisi kama wazee.''Alisema Julius Mbananje.
Hata hivyo Baltazar Momoya ambaye pia ni Mfugaji wa nyuki katika shamba la Nyuki la west Kilimanjaro ameongeza kwa kusema licha ya uwepo wa maeneo na jitihada zao binafsi bado wana uhitaji wa mitaji itakayowasaidia kurahisisha zoezi hilo la ufugaji wa Nyuki.
"Bado tunahitaji kushikwa mkono licha ya kwamba tumepatiwa wataalamu wa Nyuki na maeneo ya ufugaji wa nyuki,Mzinga mmoja wa nyuki ni takriban sh.Elfu sabini tunashindwa kumiliki mizinga ya kutosha kwa kukosa fedha za kununua mizinga hivyo inatulazimu kutumia mizinga michache tuliyo nayo TFS imetusaidia sana tunaomba wadau na Serikali pia mtushike mkono''Alisema Baltazar Momoya.
Kazi hii ya ufugaji wa nyuki licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali lakini imekuwa mkombozi kwa vijana wasio na ajira Bw.Richard Mbwebya anafafanua.
"Niliamua kuungana na wazee hawa mara baada ya kujua faida ya kujiajiri mwenyewe,uzuri ni kwamba nina elimu ya kutosha ya ufugaji Nyuki,nimekuwa nikisaidia vikundi mbali mbali vya ufugaji Nyuki hapa katika shamba la Nyuki la West Kilimanjaro na ninaifurahia sana kazi yangu kwani inanipatia kipato kinacho kidhi mahitaji yangu,nashauri vijana wenzangu kujiajiri ili kuepukana na utegemezi kwa serikali na jamii kiujumla''.
Kwa upande wa Mhifadhi msaidizi wa shamba la miti west Kilimanjaro THEOFIL LEONARD na mtaalamu wa nyuki JOEL TARIMO wanasema shamba hilo mbali na kutunza mazingira linasaidia wakazi wa eneo hilo kujikwamua kiuchumi.
"Tumekuwa tukitoa maeneo kwaajili ya kilimo pindi miti inapokuwa midogo,wakaazi wa West wamekuwa wakiyatumia maeneo hayo kwa shughuli mbali mbali za kilimo cha Viazi,maharage,Njegere,vitunguu nk.Hii imekuwa na tija sana kwao kwani tunawapatia mashamba hayo bila malipo yoyote kutoka kwao." Theofil Leonard"
"Tumeona ni bora turuhusu pia ufugaji wa nyuki ndani ya shamba la Miti la West Kilimanjaro kwani itasaidi ulinzi na kuepusha uharibifu wa miti uliozoeleka hapo awali,Kwa kuwashirikisha wananchi ndani ya Msitu ni rahisi wao kuwa walinzi kulingana na shughuwanazofanya."Ameongeza Bw.Joel.
0 comments:
Chapisha Maoni