.

.

WANANCHI MONDULI WAPEWA MSAADA WA TANI 12 ZA MAHINDI

mwandishi wetu,Monduli

  Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa Jamii( CORDs ) limetoa msaada tani 12 za mahindi ya bure kwa kaya 553 za wilaya ya Monduli mkoa Arusha, ili kukabiliana na njaa .



msaada huo umetolewa kutokana na wakazi wengi wa Monduli kukabiliwa na njaa.

Afisa Miradi wa   CORDs Martha Katua  amesema shirika hilo limetoa msaada huo baada ya kubaini Kaya nyingi kukabiliwa na uhaba wa chakula.

Katau amesema' wamegawa Tani 12 za Mahindi kwa kaya 553 katika Kata ya Mfereji Wilaya ya Monduli.

Amesema  vijiji ambavyo vimenufaika na msaada huo ni Kijiji Indonyonodo ambacho kimepatiwa Tani 6.5 kwa kugawanywa kwa Kaya 301 na Kijiji cha  Amalua Kaya 252  zimepata Tani 5.5 za Mahindi.



Mwenyekiti wa Bodi ya CORDs Yohana Ordorop alisema jamii ya wafugaji Longido inakabiliwa na njaa kutokana na ukame.

"wafugaji wanategemea kuuza mifugo ili wanunuwe chakula ila sasa ukame umeua mifugo na mingine kukonda"alisema

Kaimu Afisa Kilimo , wilaya ya Monduli Theobald Ngobya amesema wilaya hiyo inahitahi tani 28,000  za chakula.

Ngobya alisema kumekuwepo na uzalishaji mdogo wa chakula kwa misimu zaidi ya kimwili mfululizo katika wilaya hiyo hatua ambayo imesababisha upungufu wa chakula.



Amesema wilaya hiyo inaupungufu wa mahindi Tani 22,550 na maharagr Tani 7578 ili kupunguza tatizo la uhaba wa chakula katika maeneo mengi.

Jeremiah John amepongeza CORDS kuwapa msaada wa chakula kwani wanauhaba wa chakula.

John ameomba mashirika mengine  na serikali kuwasaidia.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni