.

.

UMOJA WA VIJANA UVCCM ARUSHA MJINI WAFANYA UKARABATI MADAWATI 80 NA KUOTESHA ZAIDI YA MITI 100 KATIKA KATA YA OLASITI

Na ALVIN EMMANUEL -ARUSHA.

 Jumuiya ya umoja wa Vijana Ccm wilaya ya Arusha mjini, Waadhimisha miaka 46 ya Chama mapinduzii Kwa kufanya matukio makubwa ndani ya kata ya Olasiti .



Akizingumza na dira ya maisha mwenyekiti wa umoja wa Vijana Ccm wilaya ya Arusha mjini ndugu Hassan Mndeme ameeleza kuwa  kama jumuiya  wanatambea ndani ya itifaki ya Chama Cha mapinduzii na  kusimamia ilani ya Chama Cha mapinduzi kwakusema Yale yote Ambao yamekuwa yakifanywa na serikali.



vile vile amebaniasha kuwa kama Vijana wameadhimisha siku hiyo ndani ya Kata ya Olasiti ambapo wamefanya matukio makubwa mawili ikiwemo kukarabati madawati yalio haribika ndani ya shule ya msingi Olasiti pamoja na kuotesha miti Kwa kujali mazingira ndani ya shule ya secondary ya Olasiti.



Kwa kutambua jumaiya ya Vijana ni jumuiya, inayoinganisha Jamii, Ameeleza kuwa wamejumuika Vijana mbali mbali ndani ya Arusha mjini ili kuchangia nguvu kazi Kwa kufanya Kwa matendo zaidi Kwa kuonyesha sapoti Kwa serekali Kwa kurekebisha madawati yalio haribika na kurudisha  kwenye uimara wake.



Pia Alihitimisha  Kwa kushukuru Serekali ya mama Samia suluhu Hassan kutoa mchango mkubwa ndani ya wilaya ya Arusha mjini ambao wamefanikiwa kujenga mojawapo ya madarasa ya kisasa ndani ya shule ya msingi Olasiti.



Nae ndugu Alex Martin ambae ni Diwani wa kata ya Olasiti Amewashukuru umoja wa Vijana Ccm wilaya ya Arusha mjini Kwa kuzidi kufanya mambo makubwa na ya kuigiwa  Kwa kuonyesha kusapoti serekali Kwa kutumia nguvu Yao ya  Vijana Kwa kufanya shughuli mbali mbali ndani ya kata ya Olasiti.



Pia Alishukuru  serekali kuu Kwa kuwapa mchango mkubwa ndani ya kata ya Olasiti ambapo.alieeleza kuwa Wamefanyiwa mambo mengi mazuri ikiwemo ,kujengewa madarasa, Hospital, huduma ya maji na kadhalika, amebainisha kuwa wamekuwa wakinufaika sana na kazi infanyika Kwa Kasi zaidi.



Pia mwenyekiti wa Umoja Vijana Ccm kata ya Olasiti Ndugu Musa Mohamed wakati Akikabidhi madawati alieleza kuwa wamefanikiwa kukarabati zaidi ya madawati 80 ambayo itawafanya wanafunzi Zaid ya 200 kuondoka na changamoto ya kukosa madawati tofauti na hapo nyuma Jambo ambalo kama mwenyekiti wa umoja wa Vijana kata ya Olasiti anajuvunia kufanikiwa Kwa kasi hiyo kubwa.



Pia Anna Christopher mahakamuu mkuu wa shule ya msingi Olasiti Akiongea ameshukuru umoja wa Vijana Ccm kata ya Olasiti Kwa kazi kubwa walio fanya akieleza kuwa itakua ukumbusho mkubwa ndani ya shule ya msingi ya Olasiti na kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukosa madawati.



Zoezi hilo lilihitimishwa na umoja wa Vijana Ccm kata ya Olasiti wakishirikiana na Uongozi wa Vijana Ccm wilaya ya Arusha mjini Kwa kufanya ziara ndani ya shule ya secondary ya Olasiti na kuotesha miti Kwa kujali mazingira zaidi na kuonyesha  Uzalendo Kwa kufanikiwa kuotesha zaidi ya miti 100 ndani ya shule ya secondary Olasiti,,

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni