Na Alvin Emmanuel Arusha.
Uongozi wa vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Arusha idara ya Vijana Chama Cha mapinduzii Ccm ( senet) wamesema wapo tayari kuilindaa serekali Yao inayoongozwa na Raisi wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania ndugu Samia Sulluh hasani.
Akizingumza kwenye mkutano wa tawi katika chuo kikuu Cha sauti mkoani Arusha Wakati wa darasa la itikadi na uzalendo ndugu Majaliwa Ngolo ambaye ni katibu wa idara ya umoja wa Vijana Vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Arusha chama Cha Ccm aliweza kubainisha mambo kadha wa kadha yaliofanywa na serikali ,huku akieleza kuwa watawajibu wapinzani Kwa takwimu zaidi Kwa mambo yaliofanywa na ilani ya Ccm.
vile vile mwenyekiti wa umoja wa Vijana Ccm wilaya yaArusha mjini ndugu Hassan Mndeme wakati akizingumza na Vijana aliweza kubainisha mambo yanayopaswa kufwatwa na Vijana ikiwa ni pamoja na uzalendo Kwa nchi ya Tanzania.
Pia mwenyekiti wa tawi katika chuo Cha sauti Ndugu Uzale Madiba aliwashukuru Vijana wote waliyoweza kuhudhuria mkutano huo huku akibainisha kuwa wanaenda kuwa na mwanzo mpya Zaidi kuliko hapo mwanzo kutokana na Elimu waliyopata
Ikumbukwe kuwa Raisi wa jamhuri wa Muungano Tanzania Dkt Samia Sulluh Hasani mnamo January 3 / 2023 alikutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini Tanzania na kuondoa katazo la mikutano ya hadhara, hivyo Basi vyama mbalimbali vinaendelea kufanya mikutano pamoja na vikao mbali mbali vya kujijenga zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni