Na Onesmo Mbise-Arusha.
Katibu wa chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya kaskazini mwa Tanzania Bw Amani Golugwa amesema wapo tayari kumpokea Godbless Lema ambae ni mwenyekiti wa chama hicho kanda ya kaskazini na mjumbe wa kamati kuu ya chadema kesho majira ya saa sita na nusu za mchana katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA akitokea nchini kanada ambapo ameishi kwa miaka miwili.
Golugwa ameeleza hayo mapema leo hii wakati akizungumza na wandishi wa habari katika mkutano wao na vyombo vya habari jijini Arusha ambapo ameeleza kuwa katika mapokezi hayo wataongozwa na Viongozi wakuu wa chama, wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho na waliokuwa wagombea ubunge katika uchaguzi wa 2020, na viongozi mbali mbali wa kanda zote za Tanzania huku wakiongozwa na mwenyekiti Freema Mbowe.
“Tutampokea mwananchama mwenzetu Godbless Lema katika uwanja wa KIA ambapo tutaongozwa na viongozi wote wakuu wa chama, viongozi wa kanda zote za Tanzania na Zanzibar na kuelea jijini Arusha”amesema Bw Golugwa.
Aidha ameeleza Kuwa mara baada ya kumpokea Bw Godbless Lema msafara utaanza kuelekea Arusha mjini katika viwanja vya Relni, ambapo Bw Godbless Lema akiwa njiani katika eneo la kikatiti atashiriki katika zoezi la kupandisha bendera kuinua msingi na hali kadhalika katika eneo la tengeru pamoja na kituo cha elboru.
Vilevile katibu huyo ameeleza kuwa Mara baada ya msafara kuwasili katika viwanja vya Relini mwenyekiti wa kanda ya kaskazuni Bw Godbless Lema atazungumza na watanzania kuelezea yale yaliyomkuta katika safari yake ya kuelekea nchini Kanada kwa kupitia kenya.
“Mwenyekiti wetu wa kanda atakapofika katika viwanja vya relini atazungumza na watanzania huku akieleza yale yaliyomkuta katika safari yake ya kuelea kananda kwa kupitia nchini kenya”amesema Golugwa.
Hata hvyo katika mkutano huo na vyombo vya habari umehuduriwa na aliekuwa mgombea Uraid nchini Kenya katika uchaguzi ukiopita wakili na Profesa Geoge Wajakoya ambae ameeleza kuwa na yeye yupo tayari kushiriki katika mapokezi ya Mh Godbless Lema nah ii ni kutokana na urafiki wake na Mh Tundu lisu.
0 comments:
Chapisha Maoni