Mussa Juma na Onesmo Mbise,
Arusha.
Aliyekuwa Mgombea Urais nchini Kenya Profesa George Wajackoyah amewatadharisha Chadema kuwa makini na mchakato wa Katiba mpya Ili kuhakikisha wanapata Katiba bora.
Wajackoyah amesema suala la Katiba mpya linahitaji muda na maandalizi mazuri na Chadema wasifanye makosa kama walivyofanya wao nchini Kenya.
Akihutubia mkutano wa Mapokezi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini ,Godbless Lema amesema chadema inapaswa kujifunza kutoka Kenya.
Katika hotuba yake amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa Namna anavyoendesha kwa mfumo mzuri wa kidemokrasia bila Kujali Udini na Ukabila.
"Nampongeza Sana Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa Namna anavyoendesha nchi kwa kujali Democrasia nchini" Amesema Wajackoyah
Wajackoyah amemuamba Rais wa Tanzania Mama Samia Hassan kusaidia katika Kuunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili wananchi wake wawezesha kufanya biashara hata kwa kutumia Vitambulisho vyao vya utaifa.
Profesa Wajackoyah ameeleza kuwa nchi za Afrika Mashariki zinaweza kufanya biashara bila Kutozwa kodi au pengine kupunguziwa Kodi katika Biashara zao wanazozifanya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbali na hayo Wajackoyah amesema kuwa nchi zinazotumia Ukabila katika uendeshaji wa siasa zao wanaweza kujifunza kwa Rais wa Tanzania Samia Hassani kwa namna ambavyo nchi yake haitaji Ukabila Katika Siasa zake.
Profesa huyo pia amesema amejifunza mengi kutoka Chadema na ataendelea kujifunza kwani amebaini wana sera nzuri.
Picha Mbali mbali za Viongozi waliomlaki Lema zinafuata.
0 comments:
Chapisha Maoni