.

.

Hukumu ya Muslim Brotherhood kutolewa

Hukumu dhidi ya Muslim Brotherhood kutolewa
Mahakama moja katika mji wa Minya leo inatarajiwa kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu hukumu ya kifo iliyotolewa mwezi uliopita kwa wafuasi 529 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo sasa limepigwa marufuku nchini humo.
Kesi hiyo ilizua shutuma kali kutoka jamii ya kimataifa.
Watu hao walipatikana na hatia ya kumuua afisa mmoja wa polisi katika rabsha zilizozuka mwezi Agosti mwaka uliopita.
Watu hao walihukumiwa kifo kwa mara ya kwanza mwezi Machi baada ya kesi kufanyika kwa takriban saa moja.
Mawakili wa utetezi walinyimwa fursa ya kujieleza na hata mashtaka hayakutangazwa.
Baadaye kesi hiyo iliwasilishwa mbele ya mmoja ya viongozi wakuu wa kidini ili kuamuliwa tena lakini maoni yake hayakuzingatiwa.
Miongoni mwa waliohukumiwa kunyongwa ni vijana wawili wenye umri wa miaka 17, mtu mmoja mlemavu na wakili aliyewakilisha baadhi ya
washukiwa hadi alipokamatwa.
Mawakili wa washtakiwa wamesema watakata rufaa iwapo mahakama itapitisha hukumu zilizotolewa.
Baadhi ya wataalam wa maswala ya sheria wametabiri kuwa huenda kesi dhidi ya waku hao ikasikizwa tena.
Mahakama pia inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ya pili dhidi ya watu 700 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood
baadhi wakikabiliwa na mashtaka ya kuhusika katika machafuko.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni