.

.

Watu 22 wauawa kwenye shambulio la silaha CAR

Watu 22 wauawa kwenye shambulio la silaha CAR
Kwa akali watu 22 wameuawa wakiwemo viongozi 15 wa kikabila na makumi ya wengine kujeruhiwa, baada ya watu waliobeba silaha kushambulia eneo la Nanga Boguila lililoko umbali wa kilomita 450 kaskazini mwa Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
          Taarifa zinasema kuwa, madaktari watatu wasio na mipaka pia ni miongoni mwa watu waliouawa kwenye shambulio hilo la kushtukiza. Shambulio hilo limefanyika wakati viongozi wa kikabila walipokuwa wakikutana na kufanya mazungumzo na madaktari wasio na mipaka kwenye kituo cha afya cha Nanga Boguila.
          Wakati huohuo, Waziri wa Afya na masuala ya Kibinadamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amepinga hatua ya kuwaondoa Waislamu waliobakia katika kitongoji kimoja kilichoko mjini Bangui.

Marguerite Samba amesema kuwa, serikali ya Bangui haiafikiani na hatua zilizochukuliwa na Shirika la Wahajiri la Umoja wa Mataifa la kuwaondoa Waislamu mjini humo, kwa lengo la kuwaepusha na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka. Shirika hilo la kimataifa lilichukua hatua hiyo baada ya kujiri mapigano makali wiki iliyopita kati ya wanamgambo wa Anti Balaka na wanajeshi wa Ufaransa, yaliyopelekea watu saba kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.  
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni