Mafuriko mjini Dar, hali ni mbaya Dira Ya Maisha 11:03 Edit Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam nchini Tanzania amesema hali sio nzuri kutokana na kuendelea kunyesha mvua kubwa zinazosababisha mafuriko na hivyo amewataka wananchi wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina mashimo. Kamanda Kova pia amewaomba watu wapunguze mizunguko isiyo ya lazima barabarani. Takwimu zinaonyesha kuwa, takriban watu 10 wakiwemo watoto wadogo wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye jiji la Dar es salaam. Mvua hizo pia zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu yakiwemo madaraja makubwa yanayoliunganisha jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine. Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia kuhama kutoka kwenye makazi yao. Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus About Dira Ya Maisha This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel. RELATED POSTS
0 comments:
Chapisha Maoni