Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, kwa akali watu 56 wamefariki dunia na wengine 69 kujeruhiwa, kwenye ajali ya gari moshi iliyotokea katika jimbo la Katanga nchini humo. Dikanga Kazadi amesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka idadi ya vifo kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mahututi. Dikanga Kazadi ameongeza kuwa, serikali ya Kinshasa imeunda tume kwa minajili ya kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Taarifa zinasema kuwa, treni hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba abiria karibu na mji wa Likasi kabla ya kupata ajali. Mji wa Likasi uko kati ya miji yenye utajiri mkubwa wa madini ya Lubumbashi na Kolwezi. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kuna udhaifu mkubwa kwenye sekta ya mawasiliano nchini Kongo na hasa kutokana na kutokea ajali za mara kwa mara za ndege, boti na magari mosh
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 comments:
Chapisha Maoni