Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekutana na wabunge kutoka eneo lenye wakaazi wengi wa kabila la Somali na kuwahakikishia kuwa jamii yao haitalengwa katika oparesheni za usalama nchini humo.
Jana Jumatano Rais Kenyatta alikutana na wabunge 25 Waislamu wakiongozwa na kiongozi wa waliowengi bungeni Aden Duale. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu wa Rais William Ruto, Inspekta Mkuu wa Polisi David Kimaiyo na Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mutea Iringo.
Rais Kenyatta amewafahamisha Wabunge hao na kuwahakikishia kuwa oparesheni zinazoendelea za usalama hazilengi jamii yoyote na kwamba zitafanyika kwa mujibu wa sheria. Baada ya kikao hicho, Duale amezungumza na waandishi habari na kusema, 'Rais amewahakikishia viongozi wa jamii ya Wasomali na Waislamu kuwa hawatalengwa katika msako unaoendelea na kwamba serikali itashirikiana na wenyeji katika hatua za usalama.'
Huu ni mkutano wa pili wa Rais Kenyatta na viongozi Wasomali tokea oparesheni za usalama zianze wiki chache zilizopita baada ya kutokea hujuma za kigaidi katika miji ya Nairobi na Mombasa. Vikosi vya usalama vya Kenya vinalaumiwa kuwalenga Waislamu na hasa wenye asili ya Kisomali katika oparesheni za kuwasaka wafuasi wa kundi la kigaidi la Al Shaba
0 comments:
Chapisha Maoni