.

.

Mbunge Kenya: Waislamu wanahangaishwa na polisi


Mbunge Kenya: Waislamu wanahangaishwa na polisi
Mbunge wa eneo la Mandera Kaskazini huko nchini Kenya amesema kuwa, Waislamu wasio na hatia wanahangaishwa kwa makusudi kwenye operesheni ya polisi inayoendelea katika miji ya Nairobi na Mombasa. Akizungumza na Idhaa hii kwa njia ya simu, Adan Mohamed Nooru amesema vita dhidi ya ugaidi vinapaswa kuendeshwa bila ya kupendelea au kuonea jamii yoyote. Ameongeza kwamba, kamatakamata inayoendelea katika mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi inawalenga Waislamu wa jamii ya Wasomali ilihali mtaa huo una wakaazi wengine wasiokuwa Wasomali. Mbunge huyo kutoka chama cha URP ambacho ni miongoni mwa vyama vikuu kwenye muungano unaotawala wa Jubilee ametishia kusitisha uungaji mkono wake kwa serikali iwapo polisi haitotazama upya oparesheni hiyo. Vitisho kama hivyo vimetolewa pia na wabunge wengine wa Kiislamu nchini Kenya ambao wamesema kwamba vyombo vya usalama vinausawiri Uislamu kama mhimili mkuu wa ugaidi. Hata hivyo serikali ya Nairobi imekanusha kuwalenga Waislamu wasio na hatia na kusisitiza kwamba oparesheni inayoendelea inalenga kukabiliana na ugaidi na magaidi na wala sio watu wa jamii fulani au dini fulani.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni