.

.

Machar: Rais Salva Kiir lazima aondoke madarakani


Machar: Rais Salva Kiir lazima aondoke madarakaniKiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amesema kuwa amani ya kudumu haiwezi kupatikana katika nchi hiyo hadi pale Rais Salva Kiir atakapochukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu. Akizungumza kwenye mahojiano maalum na kanali ya PressTV ya hapa nchini, Machar amesema wananchi wengi wa Sudan Kusini hawana imani na serikali ya Rais Kiir na kwamba kiongozi huyo bado yuko madarakani kutokana na uungaji mkono wa kisiasa kutoka kwa viongozi wa nchi jirani za Sudan, Uganda, Kenya na Ethiopia. Riek Machar ambaye ni Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini amemtuhumu Rais wa nchi hiyo kuwa ndiye anayekwamisha mazungumzo ya amani yenye lengo la kuhitimisha vita na machafuko nchini humo. Machar amezidi kuiambia PressTV kwamba, mazungumzo yakifeli ataamrisha wapiganaji wake warudi tena kwenye medani ya vita ili kuiangusha serikali ya Rais Salva Kiir.
Mapigano kati ya waasi na serikali yalianza mwezi Disemba mwaka uliopita baada ya Rais Kiir kudai kwamba Machar alikuwa na njama za kuipindua serikali yake.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni