.

.

Rais Kikwete atunukiwa tuzo ya uongoz

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika katika sherehe kubwa iliyofanyika Washington nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Tanzania Tuzo hiyo ambayo imepokelewa, kwa niaba ya Rais Kikwete, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine kwa Rais Kikwete kwa kuwa "Kiongozi wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kwa mwaka 2013."
Pamoja na Rais Kikwete, Waafrika wengine ambao wamepewa heshima kwenye sherehe hiyo ni Dkt. Kingsley Moghalu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria na Bwana John Kennedy Opara, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mahujaji Wakristo wa Nigeria ambaye pia ni mshauri wa Rais Gooluck Jonathan wa nchi hiyo kuhusu mahusiano ya kidini nchini Nigeria.
Mwalimu akiwasaidia wanafunzi darasani Tanzania
Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Bwana Benard Membe, kwa niaba ya Rais Kikwete, na Balozi wa Nigeria katika Marekani, Profesa Ade Adefuye ambaye naye amepokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Jonathan ambaye, kama alivyo Rais Kikwete, hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo.
Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington nchini Marekani, lilimchagua Rais Kikwete kushinda Tuzo hiyo kwa mwaka 2013 baada ya wasomaji na wadau wake wengine wa Jarida hilo kuwa wamemchagua kwa njia ya kura ya maoni Rais Kikwete kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika.
Pwani ya Tanzania
Tuzo kama hiyo ilitolewa mwaka 2012 kwa Rais wa Sierra, Mheshimiwa Ernest Bai Koroma, ambaye naye alishinda Tuzo hiyo mwaka huo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Membe, Balozi Adefuye wa Nigeria katika Marekani amemwelezea kwa undani anavyomfahamu Rais Kikwete akisisitiza kuwa kiongozi huyo wa Tanzania ni kielelezo cha rika jipya la viongozi wa Afrika ambao dira na visheni yao ni maendeleo ya Bara la Afrika na wananchi wake.
Aidha, akizungumza katika hotuba yake ya utangulizi mwanzoni wa sherehe hiyo, Mchapishaji wa Jarida la African Leadership Magazine, Dkt. Ken Giami ameeleza jinsi Rais Kikwete alivyochaguliwa kwa kishindo na wasomaji na wadau wengine wa Jarida hiyo kutokana na mafanikio yake katika uendeshaji na utawala bora wa Tanzania pamoja na mafanikio yake katika ustawi wa kiuchumi wa wananchi wa Tanzania.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni