.

.

Wapinzani Kenya wakosoa operesheni ya usalama


Wapinzani Kenya wakosoa operesheni ya usalama
Nchini Kenya viongozi wa muungano wa Cord, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wamekosoa jinsi serikali inavyoendesha msako unaolenga kuwanasa washukiwa wa ugaidi nchini.Wakizungumza katika maeneo tofauti, viongozi hao walisema kuwa msako huo, unawaathiri hata raia wasiokuwa na hatia. Akizungumza na gazeti la kila siku la Taifa Leo akiwa Marekani, Odinga amesema kuwa amesikitishwa na jinsi serikali inavyoendesha operesheni ya kukabiliana na makundi ya kigaidi hususani katika mtaa wa Eastleigh, jijini Nairobi. Odinga amesema kuwa si jamii ya Wasomali pekee ndiyo inayohusishwa na vitendo vya ugaidi nchini Kenya, kwani washukiwa wa ugaidi kutoka katika jamii mbalimbali kama vile Waluo, Waluhya, Wakikuyu na jamii nyinginezo wamewahi kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya ugaidi. Wakati huohuo, Musyoka amekosoa amri  iliyotolewa hivi  majuzi ya kuwapiga risasi washukiwa wa uhalifu na kusema kuwa inakiuka katiba. Makamu huyo wa zamani wa rais wa Kenya, amesema kuwa yeye akiwa mwanasheria, hawezi kuunga mkono amri hiyo ya kuua na kuongeza kuwa mshukiwa hana hatia hadi mahakama ithibitishe vinginevyo. Amesema kuwa tatizo la ukosefu wa usalama ambalo limeikumba nchi limesababishwa na maafisa wafisadi  ambao wanalinda vizuizi vilivyoko barabarani. Hata hivyo, serikali ya Kenya Jumanne ilikanusha madai kuwa inalenga jamii ya Wasomali katika operesheni ya usalama inayoendelea nchini humo.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni