.

.

Wamisri nje ya nchi waanza kupiga kura za urais


Wamisri nje ya nchi waanza kupiga kura za urais
Uchaguzi wa rais wa Misri umeanza leo nje ya nchi ambapo zoezi hilo linafanyika katika nchi 124 duniani kwa muda wa siku 4.

 Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Ndani ya nchi hiyo Wamisri wapatao laki 6 wanaoishi nje ya nchi hiyo waliotimiza masharti wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo. Badr Abdul'atwi msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri amesema balozi zote na balozi ndogo za nchi hiyo nje ya nchi isipokuwa katika nchi zisizokuwa na uthabiti kama vile Libya zimejitayarisha kwa ajili ya uchaguzi huo.

Uchaguzi wa rais ndani ya Misri umepangwa kufanyika tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa Mei, na matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa Juni 5. Uchaguzi huo utawashirikisha wagombea wawili tu, ambao ni Abdulfattah al Sisi  aliyekuwa mkuu wa majeshi na waziri wa zamani wa ulinzi wa Misri na Hamdeen Sabahi mwanasiasa wa mrengo wa kushoto.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni