wanfunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ajtc wakisikiliza kwa umakini mtoa mada katika mafunzo ya ujasiria mali picha na onesmo mbise. |
Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha kimetoa mafunzo bora kbsa ya ujasiriamali kwa wanafunzi wake na kuwafundisha mbinu mbali mbali za kuanzisha miradi ya kibiashara yenye kudumu na kuleta mabadiliko katika maisha yao.
Akizungumza katika mafunzo hayo mkurugenzi wa mafunzo wa chuo hicho bw Jseph Mayagila
amewasisitiza wanafuni hao kuwa na macho yenye akili ambayo yanaweza kutambua fursa na kuifanyia kazi,na ili mtu awe na macho ya fursa nilazima watembee kwa faida,watambue matatizo ya jamii na kuyatatua kwa kuanzisha biashara yenye kuuza,.
Pia bw mayagila mayagila amewataka waafunzi hao kuwa na tabia ya kuzusha jambo au mambo yenye fursa kibiashara ambayo yatawaletea mafanikio kibiashara na watu wayafanye kwa lengo la kuingiza bidhaa na kuziuza ama jambo lenye kutoa huduma.
Awali ya hayo alitanguliwa na mtoa mada mwingne bw adson kagiye akiwa anazungumzia fursa mbali mbali za kibiashara wadogo wadogo ikiwa nipamoja na kununua hisa,kuandika vitabu,kuhariri vipindi au vitabu,kuwa wakala wa biashara katika makampuni mbalimbali.
Aidha katika mafunzo hayo wajasiriamali hawa watarajiwa wameweza kupata mafuno mbalimbli jinsi ya kuanzisha biashara,jinsi ya kufanya utafiti wa kibiashara,kutengeeza mtandao watu,jinsi ya kutafuta mtaji na jinsi ya kuhudumia wateja katika biashara,
Mafunzo ya ujasiriamali katika chuo hicho imekuwa ni tabia yao kutoa na kuwaelimisha wanafunzi wao juu ya kujitegemea kibiashara ambapo hadi sasa wameweza kutoa mafunzo kwa washiriki Zaidi ya 6000 tangu kuanzishwa kwa mpanguo.
0 comments:
Chapisha Maoni