Kukopa Toka Benki Au Mashirika Ya Mikopo
Benki ni sehemu moja kubwa kabisa ambayo unaweza kuitumia kuipata fedha za mtaji. Watu wenye fedha wanaweka fedha zao hapo kwa ajili ya usalama. Benki wanatumia fedha hizo kuzalisha zaidi kwakuwekeza katika sehemu mbalimbali ikiwemo kutoa mikopo kwa biashara zenye uwezo wa kurudisha kwa faida.
Unachotakiwa kuwaonesha benki ni kuwa unabishara yenye mpango mzuri na unaweza kurudisha fedha hiyo ikiwemo riba ambayo ni faida yao.
Unaweza ukaanza na kiasi kidogo tu kama Milioni 1-5 na ukiweza kurudisha kama inavyotakikana basi unakuwa umejenga uaminifu na hivyo kuwa rahisi unapoomba kwa mara nyingine.
Ukiwa katika kikundi klwabaadhi ya mashrikaya fedha ni rahisi zaidi kupata mkopo kuliko ukiwa peke yako.Ukiwa na mali kama ardhi,nyumba au hata gari unaongeza uwezekano wa kuaminika na kupewa mkopo.
Kukopa Toka Kwa Ndugu Na Marafiki
Ndugu zako au marafiki ni mojawapo ya sehemu ya kupata mkopo. Mara nyingi mikopo ya watu hawa haina masharti magumu sana,japo ni hatari kama utashindwa kurudishakama ilivyopangwa kwani utahatarisha uhusiano wako nao.
Wakati mmoja katika familia ni masikini au anakosa mtaji wa bishara kuna ndugu mwingine anafedha isiyotumika kukua na kuleta faida (Fedha iliyolala). Tafuta jinsi ya kushawishi fedha hii itumike kujizalisha na mazao ya mtaji huo uwafaidishe wote,wewe mkopaji na mwenye fedha.
Uaminifu ni kitu cha msingi sana katika kufanikisha hili. Ukiwa mtu unayeaminika ni rahisi kwa ndugu na marafiki kukuamini na fedha zao. Uaminifu ni mtaji mkubwa katika mchezo wa fedha.
Kuingia Ubia Na Wenye Fedha
Baadhi ya watu wenye fedha inawawia vigumu kuwaamini watu na fedha zao. Hawa unaweza kuwashirikisha katika utendaji na usimamizi wa biashara husika. Uza wazo lakokwao na uwashawishi waeke fedha. Kwakuwa wewe hauna fedha mchango wako utakuwa nguvu zako za kuendesha biashara hiyo (Mtendaji). Unaweza kumweka mshirika wako mwenyefedha katika maeneo ya kiuongozi hasa wa fedha ili alinde fedha zake na kujenga imani.
Njia hii ni rahisi zaidi kwani hauhitaji kulipa deni na ni rahisi mwenyefedha kuamini kwani yeye mwenyewe ni mshirika na anjua kinachofanyika.
Vikundi Vya Kuweka Na Kukopa Na Vikoba
Vikundi vya kuweka na kukopa na vile vya kuchangiana kwa madhumuni ya kukusanya fedha nyingi ya kutosha kufanya jambo kubwa kwa mmoja wa wanakikundi ni jinsi mojawapo ya kutumia fedha za watu wengine kujiendeleza.
Tengeneza mpango wa biashara ambao una faida na chukua fedha katika kikundi chako ulichojisajili. Hakikisha bishara yako inaweza kurudisha fedha kwa wakati kulingana na masharti ya kikundi chenu.
Pokea Malipo Kabla Ya Kutoa Huduma
Ili kutengeneza bidhaa za kuuza,au kununua bidhaa ili uziuze unahitaji fedha kabla. Na hili linafanya wasio na mtaji kutoendelea na mipango yao.
Mbinu hii inakuhitaji wewe kutafuta mteja kwanza kabla ya kutengeneza au kununua bidhaa. Mteja akiwa tayari amekubali kununua atatakiwa kutoa malipo kabla,kisha unanunua bidhaa kwa fedha zake na kuwauzia kwa bei ya juu ili kupata faida. Kwa namna hii basi unakuwa unatumia fedha zao wenyewe kuendesha biashara yako na kutengeneza faida.
Wateja wanahitaji kukuamini sana ilikuweza kukupa fedha kabla ya huduma.
0 comments:
Chapisha Maoni