Vikosi vya mapigano vinavyounga mkono serikali ya Libya vimesema vimedhibiti makao makuu ya wapigani wa dola la kiislam katika mji wa Sirte.
Vikosi hivyo vikiongozwa na wapiganaji wa mji jirani wa Misrata, vimesema vinadhibiti kituo cha mikutano cha Ougadougou na hospitali kuu ya Sirte, lakini bado baadhi ya wapiganaji wa kundi la dola la kiislam wapo katika makazi ya watu katika maeneo hayo. Sirte ilikua na udhibiti wa hali ya juu wa dola la kiislam.
Vikosi vinanyounga mkono serikali ya Libya vilipata usaidizi wa ndege za mashambulizi kutoka Marekani ziliombwa na serikali yao.
0 comments:
Chapisha Maoni