Mwanaharakati nchini India Irom Sharmila anakamilisha mgomo wake leo wa kukataa kula chakula kwa miaka 16 ikiwa ni adhima yake ya kupinga sheria tata ya ukatili ambapo maofisa wa jeshi wamepewa mamlaka ikiwemo kupiga risasi na kuuwa raia nchini humo, jambo ambalo ameliita ni unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mwanaharakati huyo ameachiliwa huru na anatarajia kuanza kula hii leo baada ya Mahakama katika Jimbo la Manipur lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Lakini mwezi uliopita aliiambia mahakama kwamba anataka kukatiza mgomo wake na kuanza kampeni yake kama mgombea huru katika uchaguzi ujao wa wabunge .
Mpiga picha Ian Thomas Jansen-Lonnquist alifuatilia kwa karibu safari yake katika miaka michache iliyopita.
Ameishi kipindi kirefu cha miaka 16 chini ya uangalizi wa mahakama katika Hospitali ya Mji Mkuu wa Jimbo la Manipur, Imphal, ambako alilazimishwa kunywa mchanganyiko wa madawa na maziwa ya unga ya watoto wachanga
Bi Sharmila aliachiliwa huru mwezi Agosti 2014 baada ya mahakama kukataa shitaka kwamba “anajaribu kukujiua “. Lakini alikamatwa tena siku mbili baadae baada ya kukataa kumaliza mgomo wake.
Bi Sharmila alikuwa akihudhuria Mahakama Kuu ya Manipur kila baada ya wiki mbili kurejelea msimamo wake mgomo.
Mwanaharakati huyo alivivutia vyombo vya habari vya ndani ya nchi na vya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni. Bi Sharmila alikua na ufuasi wa wanawake na makundi yanayopigania haki za kijamii katika jimboni.
About Dira Ya Maisha
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Chapisha Maoni