LINDI:
Jengo la Mahakama ya wilaya ya Lindi. |
Mahakama ya wilaya ya Lindi, imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Navanga, Halmashauri ya Mtama kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kukutwa na hatia ya kujinufaisha kingono kwa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Maria Batraine, baada ya kuridhishwa pasipo na shaka na ushahidi uliokuwa umetolewa na upande wa mashtaka.
Mshitakiwa alifanya tendo la kujinufaisha kingono na mtoto huyo Machi 20, 2022, katika eneo la Kijiji cha Navanga, Halmashauri ya Mtama,wilayani Lindi, ambapo mshtakiwa alipata mwanya huo, wakati mtoto huyo akicheza na wenzake nje ya nyumba ya jirani yake ambapo alimuita na alipoitikia wito wake akamuingiza ndani ya chumba chake kisha kujinufaisha kingono.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Hakimu Batraine alimpa mshtakiwa nafasi ya kujitetea na kuiomba Mahakama impunguzia adhabu akidai ni mkosaji kwa mara ya kwanza na kwamba anayo familia inayomtegemea wakiwemo watoto wawili, mke na mama yake mkubwa ambaye ni mlemavu wa macho.
Mshtakiwa alidai pia mke wake ni mgonjwa aliyefanyiwa operesheni ya tumbo hivi karibuni katika Hospitali ya Mission ya Nyangao, hivyo iwapo atapewa adhabu kali kutaiweka familia yake katika mazingira magumu kimaisha na kutakochangiwa na kukosa huduma kutoka kwake.
Aidha, Mahakama hiyo ya wilaya imemuongezea mshitakiwa adhabu ya kumlipa mhanga wa tukio fidia ya shilingi 200,000.
Chanzo - EATV
0 comments:
Chapisha Maoni