eliaonesmo@gmail.com
Na Jackline Lendava-Dodoma.
Bodi ya korosha Tanzania yanunua pikipiki 95 zenye thamani ya Shilingi milioni 297 kwa Maafisa ugani ngazi ya Wilaya ili waweze kuwafikia wakulima wa korosho kwa urahisi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Korosho Tanzania Bwana Francis Alfred katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu,Malengo na Mafanikio ya Bodi hiyo uliyofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.
"Jambo ambalo tulifanya kwa sasa hivi tumenunua pikipiki 95 zenye thamani ya Shilingi Milioni 297 na kuwapatia Maafisa ugani kwa lengo maafisa hawa ngazi ya Wilaya waweze kuwafikia wakulima wa korosho urahisi zaidi".
Aidha Bwana Francis amesema kuelekea msimu mpya unaoanza 14 Octoba mwaka huu wameanzisha Programu maalumu ya huduma za ugani kwa wakulima wa korosho lengo ikiwa ni kuongeza uzalishaji.
"Mwaka jana baada ya kuanzisha masoko,kwahiyo mwaka huu kwenye kuelekea msimu tumeanzisha programu maalum kuhakikisha kila mkulima anafikiwa na huduma za ugani tumefanya hivyo katika mikoa ya Ruvuma,Mtwara,lindi na Pwani ambako kuna uzalishaji mkubwa ambapo tuliwawesha Maafisa kilimo shilingi laki moja kila mmoja,yote hiyo tunahangaika kuongeza uzalishaji ikiwa ni pamoja na kuongeza maeneo mapya ya uzalishaji".
Pia amesma kuwa wameanzisha soko mahsusi yani soko la awali ili kuhakikisha wabanguaji wa ndani hawaendi kushindana kwenye minada kama hapo awali ambapo wabanguaji wa ndani walikuwa wanapitia changamoto mbalimbali.
"Katika kutatua changamoto za ubanguaji, kwa miaka 3 mfululizo sasa tumeanzisha soko mahsusi kwaajili ya watu wa ndani,soko la awali tumewawezesha wale wabanguaji wa ndani sasa hivi hawaendi kushindana kwenye minada. Hivyo wameanzisha utaratibu maalum ambao wananunua korosho moja kwa moja kutoka kwa mkulima katika ngazi ya mukusi".
Karibia asilimia 90 ya korosho zinazouzwa Kwa sasa ni ghafi na soko kubwa liko Nchini India na Vietnam na Nchi ya China kwa kiasi kidogo.
0 comments:
Chapisha Maoni