eliaonesmo@gmail.com
Na Deborah Lemmubi-Dodoma
Zaidi ya Shilingi Billion 29.8 zimetumika kwa miradi ya CSR kwenye maeneo mbalimbali kati ya mwaka 2019 hadi 2021.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji Tume ya Madini Eng Yahya Samamba wakati akitoa taarifa ya utekelezai wa majukumu na mafanikio ya tume ya Madini iliyofanyika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dodoma.
"Kwa sasa migodi haifanyi maamuzi peke yake ya miradi ipi inataka kutekeleza bali inashirikiana na mamlaka ya Serikali ya mitaa katika jukumu hilo. Zaidi ya shilingi billioni 29.8 zimetumika kwa miradi ya CSR kwenye maeneo mbalimbali kwa kipindi kati ya 2019 hadi 2021".
Aidha Eng Yahya amesema Leseni za uchimbaji mkubwa [SML] 3 zimetolewa kati ya mwaka 2020 hadi 2022 kitu ambacho hakijafanyika kwa miaka mingi iliyopita.
"Jumla ya leseni za uchimbaji mkubwa [SML] 3 zimetolewa kati ya mwaka 2020 na 2022,ifahamike kuwa uwekezaji wa miradi ya aina hiyo ina mtaji wa zaidi ya USD 100M hivyo kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Mbali na mapato vijana wa kitanzania watapata fursa za ajira katika miradi hii, Mara ya mwisho kwa nchi yetu kutoa leseni kama hizi ni takribani miaka 10 iliyopita".
Pia Tume ya Madini kupitia Wizara ya Madini kwa kushirikiana na mamlaka ya tawaa za Mikoa Nchini imefanikiwa kuanzisha jumla ya masoko ya madini 42 na vituo vidogo vya ununuzi 83 na masoko haya yalianza rasmi tarehe 17 march 2019.
Mwaka 2021 mchango wa sekta ya Madini kwenye pato la Taifa ulikuwa asilimia 7.3 kutoka asilimia 4.8 mwaka 2018 lakini lengo ni kufika asilimia 10 mwaka 2025.
0 comments:
Chapisha Maoni