Na Jackline Lendava-Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Samia Suluhu Hassan leo Hii ametoa takwimu za Sensa ya watu na makazi kuwa watanzania kwa mwaka 2022 milioni 61,741,120.
Swali hilo limejibiwa na mhe. Rais Samia katika uzinduzi wa matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi na kusema kuwa sensa ya mwaka huu imefuata vigezo vyote vya mwongozo wa kitaifa na kimataifa.
"Ninawatangazia rasmi kuwa Tanzania ina idadi ya watu wapatao milioni 61,741,120, kati ya hao watu milioni 59,851,357 wapo Tanzania Bara na watu milioni 1,889,773 wapo Tanzania Zanzibar" mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande mwingine mhe. Rais amesema mikoa yenye watu wengi zaidi ni Dar es Salaam yenye idadi ya watu Milion 5 pamoja na Mwanza yenye idadi ya watu Milion 3 ambapo kwa Tanzania wanawake asilimia 51 wanaume asilimia 49.
""Matokeo ya sensa yanaonyesha kuwa kwa Tanzania Bara mikoa yenye idadi kubwa ya watu ni Dar es Salaam ambao una watu wapatao milioni 5,830,728 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini mkoa unaofuata ni Mwanza ulio na watu milioni 3,998,072 sawa na asilimia 6"
"Kati ya watu 61,741,120 wanawake ni milioni 31,687,990 sawa na asilimia 51 tunaposema wanawake ni jeshi kubwa, wanawake ni jeshi kubwa, Wanaume ni milioni 30,531,030 sawa na asilimia 49 matokeo ya sensa ya watu na makazi yaanze kutumika katika miradi na huduma zote za maendeleo." Mhe. Rais Samia.
Aidha mhe. Rais ameongeza kuwa Tanzania kuna idadi ya majengo milion 14 kwa Tanzania Visiwani na Tanzania Bara milioni 13 na idadi hii itawasaidia viongozi kupanga maendeleo ya wananchi kwa uhakika.
Naye Rais na mwenyekiti wa wa Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hassan Ally Mwinyi aesema kuwa matokeo ya sensa yatakuwa dira ya kusimamia sera ya maendeleo.
"Ni kwa mara kwanza kuwa na mwongozo wa kitaifa wa sensa ya watu na makazi ambao utakuwa dira itakayotumiwa katika kutekeleza maendeleo ya Taifa." Dkt Hassan.
Kwa upande wake waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa
zoezi la sensa limekamilika kwa Kwa Asilimia 99.9
"Matokeo haya yatakuwa mwanzo wa utekelezaji wa sera na mwongozo wa serikali na matokeo haya yatakuwa tija kwa Taifa letu." Waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Naye makamu wa pili wa Zanzibar amesema walipata ushirikiano kutoka kwa viongozi wakuu kila mara walipohitaji msaada kuhusu sensa
Kamisaa wa sensa kwa mwaka 2022 mhe. Anne Makinda
amewashukuru viongozi wote kwa kutoa ushirikiano katika usimamizi wa zoezi la sensa hadi kukamilika kwake.
"Nawapongeze makarani na wasimamizi wote wa sensa kwa kukamilisha zoezi la sensa Hadi kukamilika kwake." Mhe. Anne Makinda.
Mtakwimu mkuu wa serikali amesema kuwa kuna uhitaji wa kutoa mafunzo katika ngazi zote za utawala kuhusu utekelezaji wa mwongozo wa sensa ya watu na makazi.
a kipindi cha miaka kumi iliyopita Tanzania ilikuwa na idadi ya watu milioni 44,928,923 kumekuwepo na ongezeko la watu milioni 16,812,197 sawa na ongezeko la asilimia 3.2 kati ya mwaka 2012 na 2022.
0 comments:
Chapisha Maoni