.

.

NELSON MANDELA ARUSHA WATENGA ZAIDI YA BILIONI NNE UJENZI WA BWENI LA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM.

 eliaonesmo@gmail.com

Na Deborah  Lemmubi-Dodoma.

Taasisi ya Africa ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo Jijini Arusha yatenga Bilioni 4.8 ujenzi Bweni la wanafunzi, Wanawake wenye watoto na Watu wenye mahitaji Maalum.

Haya yamesemwa na Makamu Mkuu wa Taasisi Prof Emmanuel Luoga wakati akielezea utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma.



"Taasisi inadhamiria kuendeleza ujenzi wa bweni la wanafunzi ikitoa kipaumbele kwa wanawake wenye watoto wadogo na wenye mahitaji maalumu. Ujenzi ulianza Oktoba 2021 ambapo kiasi cha Bilioni 1.7 kimeshatumika kati ya Bilioni 4.8 zilizotengwa kutekeleza mradi kwa awamu ya kwanza,unaotarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2023 na kuchukua wanafunzi 180.

 Bweni hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 pindi awamu zote tatu za ujenzi zitakapo kamilika. Taasi imejizatiti kuhakikisha wanafunzi wanapata malazi bora katika kampasi ya Tengeru ikiwa ni mkakati wa kusaidia kuongeza udahili hasa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi,Teknolojia na Uhandisi"


Aidha Prof Luoga amezungumzia suala la faida na manufaa ya vipaumbele vya Taasisi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwa mwaka 2022/2023.


"Taasisi yetu inazalisha watafiti na wabunifu katika viwango vya kimataifa ambao tafiti na bunifu zao zinachangia katika kutatua changamoto za Viwanda na kijamii. Kwa mfano Taasisi imezalisha viatilifu asilia ili kupambana na magonjwa ya mimea na hivyo kuongeza tija katika kilimo



Taasisi imebuni majiko sanifu yanayopunguza gharama kwa watumiaji wa nishati za mkaa na kuni. Vilele Taasisi imesaidia viwanda katika Mikoa ya Arusha,Mwanza na Kilimanjaro kuchakata maji taka ili kuzuia uharibifu wa Mazingira na kupunguza gharama uendeshaji kwa viwanda kwa viwanda hivyo katika  kusafisha maji taka. Mifano mingine ya bunifu na tafiti zenye tija kwa wananchi inapatikana katika tovuti ya Taasisi"


Pia katika kusheherekea miaka 61 ya Uhuru Taasisi inapanga kujitangaza na kutangaza muundo mpya wa utendaji na kuurithisha muundo huo bora katika vyuo vingine hapa Nchini na nje.


"Taasisi imejipanga kuufikia Umma wa Tanzania kwa kutumia mfumo mpya wenye muundo wa utendaji wenye hatua tano ambazo ni Utafiti na Ubunifu,Mafunzo ya Uzamili na Uzamivu, Huduma za Kijamii na Ushirikishwaji wa jamii, Menejiment ya Atamizi za Teknoloia na Ubiasharishaji. Muundo huo utasaidia taasisi kushirikisha jamii na viwanda katika kutafuta suluhu ya matatizo yanayowakabili"


"Taasisi yetu pia inapanga kutumia sherehe za Uhuru kama njia ya kujitangaza, kutangaza muundo mpya wa utendaji na kuurithisha muundo huo bora katika vyuo vingine hapa Nchini na nje"


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Idara Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Bwana Gerson Msigwa amesema Serikali ina mpango wa kujenga shule 26 Nchi nzima ambapo kila Mkoa utakuwa na shule moja ambazo zitasaidia watoto wakike kujifunza masomo ya Sayansi.



Dira ya Taasisi hii ni kuwa Taasisi ya Kimataifa yenye dhamira ya kufikia na kujenga ufanisi katika Sayansi,Uhandisi,Teknolojia na Ubunifu ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo endelevu barani Africa.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni