Makala ya Mwalimu Elifuraha Samboto
Ili tukio litangazwe kwenye vyombo vya habari lazima liwe na habari ndani yake;na ili habari iwe na sifa ya kutoka kwenye vyombo vya habaari lazima iwe na mambo makuu matatu jambo la kwanza ni ukweli (factual),pili maslahi kwa wengi (human interest),jambo la tatu ni matokeo chanya au hasi (impact or consequences)
Habari ikishakuwa na hizo sifa yaani kuwa na kweli ,maslahi kwa wengi na imeleta matokeo hasi au chanya basi hii inaweza kurushwa kwenye Tv na radio zetu .
Siku hizi kumekuwa na Wimbi la habari nyingi za watu kuuawa,kubakwa na wengine kufanyiwa vitendo vya kikatili kama kuumizwa miili kwakuchomwa,kukatwa ama kupigwa.
Matukio haya yanaonekana ni mengi ingawa kwa jicho la uandishi ni machache ila kuna mahali kuna tatizo linalofanya haya matukio kuonekana ni mengi.
Unaweza kutazama Tv na ukakutana na matukio ya namna hii kama 4 kwenye taarifa ya habari ya lisa; kuwa na habari za zakufanana 4 katika taarifa ya habari ya saa moja inakera na hata kufanya watu kuamini kuwa kuna matukio mengi ya aina hii.
Waandishi wa habari kwanini mnaleta haya matukio kwa wingi kwenye Tv zetu na redio zetu?
Wengi najua mtanimabia ndio kazi yenu ,kuhabarisha umma kuhusu mambo yanayotokea kila siku.
Pamoja na hayo, mimi najua kwanini mnatuletea haya matukio kila siku na kwa wingi ,jibu ni kuwa hayawasumbui kwenye kuyaripoti maana yanatokea yenyewe ninyi ni kufika tu eneo la tukio na kuriport.
Kuriport matukio haya mara kwa mara na kuona umefanya kazi ni makosa ,maana hapa hakuna kufikiria wala haigarimu muda wala pesa tofauti na nauli pekee kufika lilipotokea tukio.
Waandishi hawataki habari za kuumiza kichwa,za utafiti au za kufuatilia siku kadhaa ili kuja na kitu kamili;wanalala tu wakiamka wasikie kuna mama alijinyonga kutokana na madeni ya vikoba ,hapo anaulizia jina tu na kukusanya ushahidi kutoka kwa mashuhuda ,ndugu wa karibu na kwa kamanda wa polisi kisha anaituma kurushwa kwenye vyombo vya habari.
Fikiria habari za vijana wasio na ajira ,watoto wenye udumavu wa miili na akili ,habari za miundo mbinu mibovu madaraja na ma darasa yaliyojengwa chini ya kiwango,kaya maskini na kaya zinazokabiliwa na njaa,kwanini hamtaki kuriport hizi habari?
Kwanini hamtafiti sababu za watoto wa Mitanni amabazo zinatoafutiana kulingana na maeneo? vip habari za kilimo cha kisasa hasa ukizingatia sehemu kubwa ya wakulima wanalima kilimo cha kizamani na hivyo kupata mazao kiduchu kila mwaka?
Kwanini hamuandiki wala kuripoti habari za misitu inayofyekwa na baadhi ya watu kutengenezea mkaa kufanya makazi na kulishia mifugo?
Ni kwanini hamuandiki habari za migogoro ya ardhi ,watu kupora maeneo ya wazi na kujenga,maeneo mengi ya shule kumegwa na kuuzwa ama kumilikiwa na watu ?
Kwanini hamuandiki habari za upandaji Miti kwa kila kaya ama taasisi;wala kuandika habari za kutunza vyanzo vya maji badala yake mpo tu mnasubiri mikutano,ziara za viongozi na watu wajinyonge muandike?
Kwanini hamripoti wala kuandika habari za elimu mashuleni vyuoni mnasubiria siku ya mtihani au siku matokeo yakitoka ndio muandike?
Kwanini hamuandiki wala kuriport habari za teknolojia watu wajifunze matumizi sahihi ya teknolojia katika kuzalisha,kuunda vitu na kurahisisha maisha?
Kwanini hamtangazi habari za fursa za kujiajiri fursa za mikopo kutoka kwenye mabenki na taasisi mbaali mbali za kifedha, watu wanakufa na umaskini kwakukosa tu taarifa sahihi za kujikwamua.
Ifike mahali kabla ya mwandishi/mtangazaji hajaripoti habari au kutangaza habari ajihoji kwenye nafsi yake je habari anayotaka kurusha ina maslahi kwa watu wengi? Ina matokeo yoyote chanya ama hasi? Kama ina matokeo hasi je yataharibu watu kiasi gani? Je ni muhimu kuirusha ama anaweza kuachana nayo akatafuta nyingine yenye kujenga umma na kuufanya uelimike ama kupata njia bora za kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Habari za kubaka ,kuua,kulawiti kujiua kung’atana maskio kuchomana moto ukizitafakari utagundua hazina maslahi yoyote kwa umma mbali na kutengeneza kizazi Sugu kinachoamini kuwa hakuna jambo la ajabu;ukidaiwa jinyonge,ukikaa na katoto we sio wa kwanza kulawiti wapo wengi,mke au meme akichepuka hata ukimuua sio wa kwanza ni mambo yapo.
Lazima matukio yote mabaya na mazuri yaripotiwe yote,ila sio kwenye vyombo vya habari bali ni kwenye vyombo sahihi.
Mfano kama mume kamng’ata mkewe masikio yote kwa kuuza mazao bila idhini yake aripotiwe polisi na wao wachukue hatua ,sioni maslahi kwa taifa zima kupewa taarifa hizi maana hazijengi wala hatuwezi kushughulikia wote tatizo hilo hilo moja.
Waandishi wa habari sio lazima mkatazwe na sheria kuwa hiki msiripoti maana sheria ikisema hivyo mtasema hamna uhuru wa vyombo vya habari,hili ni jumumu lenu kuwa na uchanganuzi wa kina kwa mambo yote kabla ya kurusha chchote kwenye vyombo vya habari kusudi taifa lisilishwe matango pori.
Vyombo vya habari na waandishi kazi yenu kuripoti nafahamu vizuri hili;Il sio kila kitu kururipotiwa kwenye vyombo vya habari mengine mtachagua habari hii ni ya kuripot polisi au ni ya kuripot kwenye vyombo vya habari.
Polisi nao nafikri washughulikie baadhi ya matukio kimya kimya bila kuita vyombo vya habari kama mtu kajinyonga apelekwe akazikwe ,na aliebaka spelekwe mahakamni; kwanini taifa zima litangaziwe? Kuna maslahi gani kwa taifa kwenye tukio la mtu kujinyonga,? Hata mtu kubakwa akiisha kamtwa mtuhumiwa inatosha ashtakiwe,taifa kujua sioni faida sana naona hasara tu kuzoesha masikio matukio ya ajabu yanayotokea na inafika mahali watu wanazoea.
Waandishi /watangazaji chonde chonde andikeni habari ya kuliinua taifa habari za kutatua changamoto za kitaifa,habari za maendeleo ,habari za elimu na rasilimali za nchi ,habari za kufurahisha.
Haipendezi mtu mwenye tabu anaamka asubuhi anakutana na habari za mtu aliejinyonga kwakushindwa kulipa madeni.
Hajajua hata chai atakunywaje anasikia habari ya mtu kulawitiwa;hizi sio habari njema hata zipewe kipaumbele kwenye vyombo vya habari,tuanzie siku na habari njema ,habari za matumaini.
Elifuraha Samboto
Facebook and Instagram
0 comments:
Chapisha Maoni